Posted by GLOBAL on February 15, 2013
AWALI ya yote nichukue fursa hii kumshukuru Mungu ambaye ameniwezesha kuiona siku hii ya leo nikiwa bukheri wa afya.
Baada ya shukrani hizo sasa nigeukie katika sehemu ya pili ya makala haya nikizungumzia madhara ya mwanafunzi kujihusisha na masuala ya mapenzi.
Mwanafunzi ambaye anataka mafanikio ya kimasomo lazima ayape kisogo masuala ya mapenzi kwa lengo la kutoitwika akili mzigo hasa kwa watoto wa kike ambao ni waitikiaji wa kauli za wavulana.
Hatukatai kwamba zipo faida kadha wa kadha za kufanya mapenzi kwa afya ya mwili wa binadamu lakini faida hizi ni kwa wale ambao wanastahili na si wanafunzi ambao wanatakiwa kutumia muda wao mwingi kwenye masomo na si kufikiria mapenzi.
Mapenzi kwa mwanafunzi yana hasara nyingi lakini leo nitagusia zile kuu mbili. Kwanza, mapenzi yanapokuwa moto huteka hisia na kumfanya msomi atumie muda mwingi kuwaza juu ya mahaba na hivyo kuufanya ubongo uone kuwa mapenzi ni kitu muhimu na hivyo kujituma kuhifadhi mambo ya mapenzi kuliko masomo.
Jambo la pili ni machungu ya mapenzi hasa kunapokuwepo mifarakano, mfano kuachwa, kusalitiwa, kuudhiwa, kugombana na migogoro yote ya kimapenzi ambayo husababisha msongo wa mawazo na kumfanya mwanafunzi ashindwe kuwekeza akili yake kwenye masomo kwa kiwango kinachotakiwa.
Hivyo basi, inashauriwa mwanafunzi asijihusishe kabisa na mapenzi. Asome kwanza, apate kazi yake na baada ya hapo anaweza sasa kumtafuta yule ambaye ataingia naye kwenye maisha ya ndoa.
Kumbuka wengi waliojihusisha na mapenzi wakiwa wanasoma waliishia kufeli mitihani yao, kuambukizwa magonjwa ya zinaa na wengine kubebeshwa mimba.
Sidhani kama wewe unataka kuwa miongoni mwao. Tumia muda na akili yako yote kwa sasa katika elimu kama kweli unataka kuja kuwa na maisha mazuri hapo baadaye.
Kufuata mkumbo si kuzuri, ukiwaona wale ambao ni malimbukeni wanaodhani kuwa na mpenzi ni sifa au ujanja, wapuuze kisha chukua madaftari yako ukajisomee.
Tambua kuwa hao ambao sasa wanaona kuwa na wapenzi ni sifa wakishakutana na ile shubiri ya mapenzi huishia kujuta.

Post a Comment