Mama aliniambia "mwanangu, usikubali hata siku moja kuwa mchawi. Babu yako alinilazimisha kunirithisha mikoba yake nikakataa, amedai kuwa mizimu imekupenda. Yupo katika harakati za kuniua kwa sababu ya kumpinga wewe kuwa mchawi" niliumizwa sana na taarifa hiyo. Mama alikuwa akiongea machozi yakimtiririka. Nilimbembelea mama huku nikimuhakikishia kuwa siwezi kuwa mchawi. Mama aliniambia "mwanangu muheshimu sana huyu mzee unayeishi naye" nikamuuliza "mzee? yupi!" sikuweza kutambua kama alikuwa akimzungumzia baba. Ainiambia "mzee Nyegezi, si baba yakoe Bella, ni mwanaume aliyeyaokoa maisha yangu baada ya mume wangu wa kwanza kutolewa kafara na babu yako" nililia sana nililia kwa uchungu kwa sababu sikujua babu yangu angekuwa na roho ya kinyama kiasi kile. Amuuwe mwanaye kwasababu ya uchawi? Kafara? Kwa faida gani? Unyama ulioje? Nilimchukia babu kwa kuninyima haki ya kumjua baba yangu na mimi kulelewa na baba wa kambo. Mama aliniambia tena "mwanangu mzee Nyegezi atakulea vyema kama baba yako mzazi. Nina uhakika sina siku saba duniani, lakini nitakapokufa usisahau kusoma kwa bidii na usikubali kuwa mchawi" alinyanyuka na kuondoka. Nilichokuwa nikisoma kikatumbukia nyongo hata wimbo wa Ben po haukuwa mtamu kama nilivyokuwa nikiupenda siku zote. Niliitupa ipod yangu mbali na nilipolala, nikapitiwa na usingizi ulioletwa na kuia sana.
......
TUFUATANE JIONI TUJUE NINI KITAMPATA MAMA YAKE BELLA KABLA YA HIZO SIKU SABA
TUFUATANE JIONI TUJUE NINI KITAMPATA MAMA YAKE BELLA KABLA YA HIZO SIKU SABA
Post a Comment