Games

LATEST UPDATES
Showing posts with label kimataifa. Show all posts
Showing posts with label kimataifa. Show all posts

Monday, March 21, 2016

MWANAHABARI ALIYETEKWA AELEZA KILA KITU KUHUSU TUKIO HILO

SALMA Said, Mwandishi wa Habari wa Shirika la Utangazaji la Ujerumani (DW) pia Gazeti la Mwananchi amesema, licha ya kutekwa na kuteswa hatorudi nyuma, anaandika Regina Mkondo.

Amesema, kazi yake ya uandishi na kuripoti matukio mbalimbali ikiwa ni pamoja na yale yanayovunja haki za binadamu itaendelea kama kawaida.

Amesema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ikiwa ni siku mbili baada ya kutekwa na watu ambao hawakujitambulisha akiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julisu Nyerere.

“Kupigwa kwangu sio kitu kikubwa zaidi ya kuzuiwa kuandika na kuripoti habari, sababu naamini wananchi walitarajia kusikia ripoti zangu na kufahamu hali halisi inayoendelea visiwani Zanzibar,” amesema Salma.

Amesema, wiki mbili kabla ya kufanyika uchaguzi wa marudio visiwani Zanzibar alipata ujumbe wa vitisho uliomtaka kujihadhari juu ya kazi anazozifanya za kuripoti taarifa ambazo ziliwakera baadhi ya viongozi.

“Kama mnavyojua tangu kufutwa matokeo ya uchaguzi mkuu wa Zanzibar Oktoba 25, 2015 kulitokea mambo mabaya katikati ikiwemo ukiukwaji wa haki za binadamu kama kupigwa, kutekwa na kutupwa nje ya mji,” amesema Salma na kuongeza;

“Sisi tunaoijua Zanzibar tunayaona haya, kuna baadhi ya mambo hayaripotiwi na vyombo vya habari kwasababu ya vyombo hivyo kupewa vitisho, lakini kwa waandishi wanaoripoti katika vyombo vya nje kama Aljazeera walifanikiwa kuandaa dokumentari ya matukio hayo.”

Salma amesema, watekaji hao walimwambia kuwa ametekwa ili kuzuiwa kutoendelea kuripoti habari za uchaguzi.
“Awali nilipigiwa simu na kutumiwa ujumbe wa simu wa kunionya, nilikuwa nafuatwa hadi ofisini kwangu, kuna siku nilifukuzwa na gari hadi nikadondoka chini,” amesema.
“Nimeteswa kwasbabau ya kazi zangu za kutaka kutetea wananchi wenzangu na nchi yangu, kuna siku nilihoji juu ya fedha kiasi cha biloni 7 zilizotumika kwa ajili ya uchaguzi wa marudio, nahisi iliwakera baadhi ya watawala,” amesema.
Salma amewataka waandishi wa habari kuacha kuandika habari za kufurahisha baadhi ya watu huku wakiumiza wananchi bali waandike habari ambazo zinaeleza matatizo ya jamii.
“Kama mwandishi ni jukumu langu la kuhakikisha kuwa natoa msaada kwa jamii kupitia taaluma yangu, nchi yetu ina matatizo mengi yanayohitaji kuripotiwa ili viongozi wayajue na kuyatatua,” amesema.
Amewataka waandishi wa habari kuwa na umoja na kuacha kuwakashfu baadhi ya waandishi wanaopata shida kama alizopata yeye.

credit: Fullhabari

Saturday, February 28, 2015

Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, kesho atafanya sherehe kubwa ya kutimiza miaka 91

Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, kesho atafanya sherehe kubwa ya kutimiza miaka 91 kwa kuchinja tembo wawili. Sherehe hizo zitafanyika kwenye mji wa Victoria Falls na zinaandaliwa na chama tawala ZANU-PF kinataka kukusanya dola za Kimarekani milioni 1 kwa ajili ya sherehe ya kesho. Wageni wapatao 20,000 wanatarajiwa kuhudhuria. Hata hivyo, mashirika ya kutetea ulinzi wa wanyama pori yamemkosoa Mugabe, wakisema haiwezekani akakemea uharamia wakati yeye mwenyewe anaamuru wanyamapori wachinjwe. Pamoja na hayo baadhi ya raia wa Zimbabwe wanakerwa na uamuzi wa rais wao kufanya sherehe kubwa kama hiyo, wakati wananchi wake wengi ni maskini.
credit: DW

Thursday, February 26, 2015

ushauri wa 50 CENT kuhusu bifu la wayne na birdman... 50 Cent Warns “Stay out of Lil Wayne & Birdman’s Cash Money Drama”



Lil Wayne and Birdman might not be speaking to each other and act as though the situation is irretrievable but 50 Cent, in an interview with MTV News, said he is sure they will eventually make up and that the situation will “work itself out.” Later in the interview, he also said: I hate when personal things become public, because everyone speculates on things that they don’t really know about. I just know that they had a father and son relationship, and that could easily be something they communicate between the two of them, and resolve instead of having everybody else involved in it.” The much-publicized legal battle between the rapper and the co-founder of Cash Money Records has turned up a notch in recent weeks, but 50 Cent doesn’t think this is reason enough for others to get involved. He believes that those outside of the matter should watch their words, and compared Lil Wayne and Birdman's relationship to a daughter and mother in terms of closeness. When they forgive each other – and 50 Cent is entirely confident they will – they may not forgive the outsiders who offered their unwanted opinions on this delicate moment of their personal and professional lives.

Saturday, February 14, 2015

Matokeo ya CSEE na QT 2014

Matokeo ya kidato cha nne mwaka 2014 yametoka bofya hapa

Friday, March 8, 2013

HII NDIO TWEET YA CCM YENYE KIINGEREZA KIBOVU.....WAKENYA WAIGEUZA KITUKO


 Chini ni Baadhi ya Comments ziliandikwa na wadau baada ya Tweet hiyo:

>This is very disappointing and the reason why there are many Division 0's!! 

>Mhhh so sad, its rather unfortunate aki, they should be banned from writing English comments, this is a serious offence to the language..lol

>No way could this be his Nyumba Ndogo coz seriously this is not serious at all. A disgrace once again to Tanzania. 

> Did ccm really tweet this?!.. no wonder they are not serious... 
 
kwa hisani ya Mpekuzi 

Wednesday, February 13, 2013

ALIYEMUUA OSAMA AFUNGUKA

RISASI tatu zilimmaliza Osama bin Laden na kuandika historia.Karibu miaka miwili sasa, baada ya kimya na siri ya namna mauaji hayo yalivyofanyika, siri iliyofichwa imewekwa wazi kuhusu namna Osama alivyowapa kiwewe askari waliomvamia nyumbani kwake ambao walishindwa kumkamata akiwa hai tofauti na dhamira ya awali.

Askari aliyetekeleza mauaji hayo, tayari amefunguka na kueleza kwamba mshtuko alioupata alipokutana uso kwa uso na kiongozi huyo ulimsukuma kutekeleza mauaji yake.

“Nilimpiga risasi tatu. Nilimshuhudia akiwa amekufa ulimi nje. Nilimwona namna alivyokuwa akikata pumzi yake ya mwisho. Niliuliza akilini: Hivi hili ni jambo jema au ni jambo baya kabisa kuwahi kulifanya katika maisha yangu?”anaeleza askari huyo.

Askari huyo ambaye alipewa jina la the Shooter “mdunguaji” amesema hawakuwa na uhakika wa kumshinda, hadi walipofanikiwa kumtia nguvuni akiwa chumbani kwake katika uvamizi uliofanyika usiku wa manane.

Operesheni hiyo ilifanyika Mei 2, 2011 baada ya maandalizi yaliyowawezesha askari sita wa Marekani kumvamia kiongozi huyo wa kikundi la Al Qaeda aliyekuwa akisakwa kwa gharama zote na Marekani akiwa katika makazi yake huko Jalallabbad, Pakistan.

BAADA YA PAPA KUTANGAZA KUJIUZULU RADI YAPIGA KANISA


Je! Hii ni ishara kutoka kwa Mungu? Sababu amini usiamini saa kadhaa baada ya Papa Benedict XVI kutangaza kuwa atajiuzulu radi kubwa ilipiga kwenye kanisa la St Peter’s Basilica.

Pope+Benedict+XVI+Pope+Benedict+XVI+arrives+9SBA5IV2gxel
Papa Benedict aliwashtua mabilioni ya waumini wa kanisa katoliki duniani kwa kutangaza kuwa atajiuzulu mwishoni mwa mwezi huu.
Papa huyo mwenye miaka 85 amekuwa kiongozi wa kanisa hilo tangu mwaka 2005. 

SOURCE:EDDIE SURCE

Tuesday, February 12, 2013

Micro Chip Implant Coming March 23, 2013



The New Health Care (Obama care) law H.R. 3590 Also HR 4872 requires all US citizens to
 have the RIFD implanted

This evil plan is being launched by America. its a micro chip injected in your hand. it will contain all your personal data heath and bank accounts etc. its also a GPS device being monitored. they can deactivate it at any time if they find you suspicious or not loyal to their government or go against them or their system and you will lose everything you ever had. soon this device will be made common just like they did credit cards, turning paper money into digital money. means nothing is physically in your hand. it will be made a must for every citizen with time according to their plan and then they will spread it outside America so they can monitor and control as many people as they can and turn them into slaves with their digital technologies.

this device is the future or slavery

BEWARE of this EVIL DEVICE. if you don't believe me do your own research before you come to argue or debate.

warn more people create this awareness do more research on your own and save yourself from this NEW DEVILRY.



Monday, February 11, 2013

PAPA BENEDICT XVI AJIUZULU

Kwa habari zilizotufikia hivi punde zinasema Papa Benedict XVI (85) ajiuzulu wadhifa wake.
Ikiwa ni mara ya kwanza kwa kiongozi wa wadhifa huo kufanya hivyo kwa miaka 600 iliyopita, Papa Benedict XVI amejiuzulu kwa sababu aliyoitoa mwenyewe kuwa ni kutokana na umri.
Na ataachia madaraka February 28 na Papa mwingine atachaguliwa Machi. ''Baada ya kutafakari umri wangu sasa hainiruhusu kuendelea katika wadhifa huu kutokana na mabadiliko ya kiimani kwa mujibu wa Mtakatifu Peter...'' alisema Mtakatifu Benedict (85).
Papa wa mwisho kujiuzulu alikua ni Papa Gregory ambaye alijiuzulu mwaka 1415 kutokana na mgawanyiko wa kidini katika nchi za magharibi

Friday, February 8, 2013

Hofu ya ghasia katika uchaguzi wa Kenya



Mamia walifariki na maelfu kuachwa bila makao kufuatia ghasia hizo
Shirika la kutetea haki za binadamu la, Human Rights Watch limeonya kuwa uchaguzi mkuu wa mwezi ujao, nchini Kenya huenda tena ukakumbwa na ghasia.
Kwa mujibu wa shirika hilo, maafisa wa serikali wamekosa kuchukulia kwa uzito sababu zilizosababisha ghasia za mwaka 2007, na kuweza kuzishughulikia. Maelfu ya watu waliuawa kwenye ghasia hizo.
Shirika hilo linasema kuwa serikali ya Kenya bado haijafanya mageuzi muhimu, na imekosa kushughulikia vyanzo vya ghasia nchini humo.
Limeelezea mfano wa ghasia za kikabila ambazo zimekuwa zikiendelea kama zile zilizoshuhudiwa Tana River, ukosefu wa mageuzi katika idara ya polisi, pamoja na kukosa kushughulikia maswala ya ardhi ambayo yamekuwa sababu kuu ya mizozo katika nchi hiyo.
Pia serikali imekosa kuwachukulia hatua washukiwa wa ubakaji, mauaji na ghasia nchini humo.
Shirika hilo linadai kuwa jamii fulani tayari zimeanza kujihami kwa hofu ya mashambulizi kabla ya uchaguzi mkuu likisema kuwa madai haya yanaweza kuthibitshwa kwa sababu ya taarifa zilizokusanywa na mashirika mengine yasiyo ya kiserikali.
Aliyekuwa kiongozi wa mashtaka katika mahakama ya ICC Luis Moreno Ocampo aliwashtakiwa washukiwa wakuu wa ghasia hizo
Kwenye ripoti ya shirika hilo, katika baadhi ya sehemu za nchi kuna hali ya wasiwasi na hofu ya ghasia.
Ghasia zilizotokea wakati wa uchaguzi wa 2007 na 2008 zilitikisa sifa ya Kenya iliyokuwa inatazamiwa kama nchi thabiti na mfano mzuri kwa Afrika Mashariki, wakati kilichoanza kama vurugu la kisiasa kugeuka na kuwa ghasia za kikabila zilizosababisha vifo vya watu 1,200 na kuwaacha wengine 600,000 bila makao.
Wasiwasi hasa umeongezeka kwa sababu ya kesi za washukiwa wa ghasia za baada ya uchaguzi huo zinazotarajiwa kuanza kusikilizwa katika mahakama ya Hague.

Daktari abaka mgonjwa

ACCRA, Ghana
POLISI nchini Ghana wamemkamata dokta anayehusika na masuala ya oparesheni za kusafisha vizazi (abortion), baada ya kutuhumiwa kumbaka mwanamke aliyefika katika kituo chake kwa ajili ya kusafishwa ujauzito wake.
Daktari huyo Joshua Dran anaaminika kubaka maelfu ya wanawake kutokana na idadi kubwa ya wanawake ambao wamejitokeza hivi sasa wakidai kufanyiwa vitendo hivyo na daktari huyo ambaye huwaomba kufanya ngono ndipo afungue mifereji ya uzazi kwa ajili
ya kusafishwa.
"Kwa upande wake kulikuwa na bei maalum ya maelewano kwa ajili ya utoaji mimba. Zaidi ada yake ilikuwa ni kati ya pesa ya Ghana yenye thamani ya ¢50 na ¢100 ambayo aliichukua kabla ya oparesheni husika.
Kwa wateja wazuri kulikuwa na malipo ya ziada, daktari huyu alihitaji ngono kabla ya kumsafisha mgonjwa, baadhi ya vyombo vya habari nchini Ghana vimeripoti.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo, Dr Joshua Dran amekanusha madai hayo, lakini alishangazwa na video ambayo iliwekwa na wapelelezi wa kesi hiyo iliyomwonyesha yeye akimtendea mgonjwa wake kitendo hicho kabla ya kumtoa mimba katika hospitali yake.
Dran anaendesha klinic ya Universal Mission Clinic iliyopo Madina mjini Accra. Kiongozi mpelelezi katika kesi hiyo Anas Aremeyaw Anas,aliwaambia waandishi wa habari kuwa "tulipokea kesi nyingi kutoka kwa huyu bwana na alikuwa akitoa mimba za wanawake kinyume cha sheria za nchi na suala hilo limepelekea vifo vya watoto wengi pamoja na matatizo ya ugumba na hata wanawake wenyewe kufariki baadaye" alisema Anas.

Thursday, February 7, 2013

Wanawake wanavyoondolewa mfuko wa uzazi India


 6 Februari, 2013 - Saa 10:45 GMT
Takriban asilimia tisini ya wanwake katika kijji kimoja inasemekana wameondolewa mfuko wao wa uzazi
Wakereketwa wa haki za kibinadamu wanasema kuwa maelfu ya wanawake wamekuwa wakiondolewa mfuko wa uzazi kwa ulaghai ambapo wanadanganywa kuwa watashikwa na saratani iwapo hawafanyiwi hivyo katika kliniki za kibinafsi.
Ifuatayo ni taarifa ya Jill Mcgivering ikisimuliwa na Wanyama wa Chebusiri.

Zote hizo zinajaza pengo la mfumo duni wa serikali hususan katika maeneo ya vijijini.Kuongezeka kwa visa vya wanawake kuondolewa mfuko wa uzazi, ni kutokana na ongezeko la kliniki na hospitali za kibinafsi katika miaka ya hivi karibuni.
Wanaharakati wanataka hospitali hizo kuchunguzwa na hata kuwekewa sheria za utenda kazi ili kuhakikisha kuwa haziwanyanyasi akina mama maskini.
Daktari Narendra Gupta anayefanya kazi katika shirika moja lisilo la kiserikali, Prayas anasema kuwa madaktari wa kibinafsi, wameona fursa ya kutengeza pesa kwa haraka.
Anaelezea kuwa kuna mbinu nyingi tu ambazo, mfuko wa uzazi unaweza kuondolewa bila upasuaji, na kwamba hiyo inapaswa kuwa tu njia ya mwisho katika matibabu yoyote.
Mmjoa wa wanawake walioondolewa mfuko wao wa uzazi
Baada ya kuondoa mfuko wa uzazi huwa ni vigumu kuthibitisha kuwa operesheni hiyo haikuwa budi kufanywa.
Lakini jambo la kushangaza ni kuwa wasichana wadogo wanaondolewa mfuko huo baada ya madakrati kuwatisha kuwa watapata saratani ikiwa hautaondolewa.
Waziri wa ustawi wa vijijini Jairam Ramesh, anasema kuwa changamoto kubwa ni kuwa mfumo wa serikali umeporomoka na kwamba watu hulazimika kwenda katika hospitali za kibinfasi,
Anasema kuwa kwa hilo watu hulazimika kutumia pesa nyingi sana na hata kupata matibabu wasiyoyahitaji.

Utulivu Tunisia baada ya mauaji

7 Februari, 2013 - Saa 07:58 GMT
Inaarifgiwa polisi mmoja aliuawa kwenye maandamano hayo
Kumekuwa na utulivu mjini Tunis, Tunisia usiku kucha baada ya siku moja ya vurugu kufuatia mauaji ya mwanasiasa mashuhuri wa upinzani Shokri Belaid.
Waziri Mkuu wa Tunisia, Hamadi Jebali, amesema ataunda Serikali ya watalamu kufuatia mauaji ya Belaid.
Maelfi ya waandamanaji waitaka serikali tawala kujiuzulu kuhusiana na mauaji hayo.
Lakini mmoja wa viongozi wa serikali alilaani mauaji hayo akiyataja kuwa kitendo cha uoga na kuwa wale waliomuua kiongozi huyo hawatafanikiwa kusababisha vurugu Tunisia.
Mauaji ya Bwana Belaidi, ambaye amekuwa mkosoaji mkuu wa Serikali yalisababaisha ghasia katika miji kadhaa nchini. Waandishi wa habari kutoka eneo hilo wanasema kufikia sasa afisaa mmoja wa polisi ameuliwa na waandamanaji hao.
Jamaa za marafiki za marehemu Shokri Belaid
Akihutubia taifa katika matangazo ya moja kwa moja katika runinga Bwana Jebali alisema kuwa Serikali hiyo itaendelea kwa muda bila mwelekeo wa vyama hadi Uchaguzi Mkuu utakapofanywa.
Maelfu ya waandamanaji walikuwa wametoa wito kujiuzulu kwa chama kinachotawala cha Kiislamu cha ENNAHDA kufuatia mauaji ya Belaid.
Muungano wa vyama vya kiraia uliokuwa mwanachama wa serikali ya muungano, uliondoka Serikalini na kuitisha mgomo wa taifa lote.

Thursday, January 31, 2013

MTANGAZAJI WA REDIO WA TANZANIA AKAMTWA NA MADAWA YA KULEVYA NCHINI KENYA





Hivi karibuni mamlaka nchini Kenya zilikamata madawa ya kulevya aina ya heroin yenye uzito wa kilo 5.44.

Msemaji wa mamlaka ya mapato nchini Kenya (KRA) Kennedy Onyonyi amesema madawa hayo yalikamatwa yakiwa na mtanzaniaSaraphia Peter Shirima, Jan. 23 alipokuwa akijaribu kuvusha madawa hayo kupitia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta.


Mamlaka hiyo imesema Saraphia sio mwanafunzi bali ni mtangazaji wa radio nchini Tanzania.Onyonyi alisema mtangazaji huyo ana kibali cha kuishi nchiini Sweden kwa miaka miwili kitakachoisha ” Nov. 28, 2014.

Madawa hayo yana gharama ya dola za kimarekani 150,000 ambapo mtuhumiwa huyo alikuwa akiyasafirisha kuyapeleka Budapest, Hungary.

Monday, January 28, 2013

Maafa katika ukumbi wa densi Brazil

28 Januari, 2013 - Saa 09:07 GMT
Wengi wa waliofariki wanaaminika kuwa kati ya miaka 16 na 20
Raia wa Brazili wanaomboleza vifo vya watu mia mbili thelathini na watatu waliofariki dunia katika ajali ya moto iliyotokea kwenye ukumbi wa muziki katika mji wa kusini wa Santa Maria.
Maafisa wanasema kuwa wengi wa waathiriwa walikuwa ni wanafunzi waliokufa baada ya kushindwa kupumua kutokana na moshi mkubwa .
Wengine zaidi ya mia moja wanapata matibabu hospitalini . Serikali ya Brazil imetangaza siku tatu za maombolezo . Taarifa zinasema kuwa moto huo ulianza wakati waimbaji wa bendi moja walipowasha fataki.
Maswali sasa yamekuwa yakiulizwa kuhusu usalama wa kumbui za starehe, huku kukiwa na madai kuwa cheti cha huduma za zima moto kilikuwa kimepitwa na wakati. Hili ni jana kubwa la moto kuwahi kuikumba Brazil kwa zaidi ya miongo mitano
Familia za waathiriwa wamekuwa wakiomboleza juu ya majeneza za jamaa zao katika ukumbi wa mamozezi ambao unatuimika kama jumba la kuhifadhia maiti.
Kwa sababu ya heshima kwa waliofariki, serikali iliakhirisha sherehe iliyotarajiwa kufanyika leo Jumatatu katika mji mkuu, Brasilia, kuadhimisha siku 500, kabla ya kombe la dunia kungo'a nagna nchini humo mwaka ujao.
Mazishi ya kwanza mjini Santa Maria yanatarajiwa kufanyika leo , kwa mujibu wa magazeti ya nchi humo.
Maafisa wa utawala wametoa majina ya waathiriwa hao,230 huku maiti watatu wakisalia kutotambuliwa.
Kulingana na taarifa za kituo cha televisheni cha Globo,wengi wa waathiriwa walikuwa kati ya umri wa miaka16 na 20.
Zaidi ya watu 100 wanapokea matibabu baada ya kushindwa kupumua kutokana na moshi mkubwa.

Uwanja wa ndegeTimbuktu wadhibitiwa

28 Januari, 2013 - Saa 09:13 GMT
Wapiganaji nje ya  mji wa Timbuktu
Wanajeshi wa Ufaransa, nchuini Mali, wameweza kudhibiti uwanja wa ndege katika mji muhimu wa Timbuktu.
Kwa mujibu wa afisaa majeshi ya hayo, waliudhubiti mji huo bila upinzani kutoka kwa wapiganaji wa kiisilamu.
Wanajeshi wa Mali na Ufaransa, wamekuwa wakipigana kuelezea Kaskazini mwa nchi dhidi ya wapiganaji wa kiisilamu.
Siku ya Jumamosi , waliuteka mji wa Gao, mji wenye idadi kubwa ya watu nchini Mali.
Maelfu ya watu walikusanyika kwenye barabara za mji kusherehekea kuwasili kwa wanajeshi hao.
Wapiganaji wa kiisilamu waliteka eneo la Kaskazini mwa nchi mwaka jana lakini wamekuwa wakishindwa tangu majeshi ya Ufaransa kuanza kuwashambulia mapema mwezi huu.
Mwandishi wa BBC nchini Mali anasema Wafaransa wanatarajiwa kuikomboa Timbuktu bila ya tatizo.
Ndege za Ufaransa piya zimeshambulia mji wa Kidal ambako ndiko wapiganaji walianza uvamizi wao mwezi Machi mwaka jana.
Jumamosi wanajeshi wa Ufaransa na Mali waliukomboa mji wa Gao uliokuwa ngome ya wapiganaji.
Na Mali ndio swala muhimu linalojadiliwa kati ya viongozi wa nchi za Umoja wa Afrika, AU, wanaokutana mjini Addis Ababa, Ethiopia.
Sasa nchi zaidi za Afrika zinatarajiwa kuchangia wanajeshi katika kikosi cha kimataifa kitachokwenda Mali, mbali ya wale walioshafika nchini humo.

Upinzani wakataa mazungumzo Misri

 28 Januari, 2013 - Saa 15:08 GMT
Serikali ya rais Morsi inakabiliwa na upinzani mkali
Kundi kubwa zaidi la upinzani nchini Misri limesema halitahudhuria mazungumzo yanayoandaliwa na Rais Mohamed Morsi hadi pale masharti yatakapotimizwa.
Mkutano huo ulinuia kumaliza machafuko ambayo yamekuwa yakiendelea katika miji kadhaa katika siku za hivi karibuni.
Awali Rais Morsey alitangaza hali ya hatari ya muda wa mwezi mzima katika miji ya Port Said, Suez na Ismailiya kufuatia siku kadhaa ya maandamano na fujo.
Amesema kuwa pia ameweka amri ya kutotoka nje usiku kucha. Kiongozi wa kundi la upinzani la Free Egyptians Party, Dr Ahmed Saeed, ameaimbia BBC kuwa rais Mosri anapaswa kufanya juhudi zaidi kurejesha imani ya wananchi.
Mapema leo Rais wa Misri Mohammed Morsi ametangaza hali ya tahadhari katika miji ya Port Said, Suez na Ismalia baada ya siku kadhaa za machafuko makali.
Kuanzia Jumatatu na kwa siku 30 zijazo watu hawatakubaliwa kutoka nje kati ya saa 21:00 na 06:00, alisema alipohutubia taifa.
"Huwa kwa kawaida napinga hali za tahadhari, lakini ilibidi niwalinde wananchi na kukomesha umwagikaji damu basi ikanabidi nifanye hivyo,” rais alisema.
Takriban watu 33 people walikufa mnamo wikiendi huko Port Said, ambapo uamuzi wa mahakama ulisababisha vurugu kuzuka.
Kutoridhika na uongozi wa Bwana Morsi's kulizua fujo kwingine nchini.
Katika mji mkuu wa Cairo, waadamanaji wailokuwa wanaipinga serikali walipambana na vikosi vya ulinzi karibu Uwanja wa Tahrir kwa siku ya nne mfululizo.

Upinzani

Upinzani unamlaumu Morsi kwa kutawala kimabavu na kuipa kipaumbele katiba mpya ambayo hailindi kikamilfu haki za kuabudu wala za maoni.
Serikali pia imelaumiwa kwa kutodhibiti hali ya uchumi, inayozidi kuzorota.
Bwana Morsi alisema kwamba angechukua hatua zaidi "kwa ajili ya Misri" na kwamba ilikuwa "wajibu wake" kama rais kufanya hivyo.
Vuru katika mji wa Portland
Aidha, aliwaalika viongozi wa kisiasa wakutane "katika majadiliano ya kitaifa " mnamo Jumatatu.
Ingawaje muungano mkubwa zaidi wa vyama pinzani nchini Misri, National Salvation Front, uliuunga mkono mualiko huo, ulilaumu sera za Morsi kwa kuzua vurugu.
Vurugu zilizuka Port Said baada ya mahakama kuwahukumu watu 21 kifo kwa kuhusika na fujo baada ya mechi ya kandanda Februari 2012.

Sunday, January 27, 2013

Soko la Bujumbura lateketea


Nchini Burundi soko kuu la mji mkuu Bujumbura limeteketea kwenye moto asubuhi mapema ya Jumapili.

Bujumbura, Burundi
Soko hilo ndilo kubwa kuliko yote nchini humo.
Sababu za kuzuka moto huo hazijajulikani bado.
Wafanyabiashara wamelaani kuchelewa kwa shughuli za uokozi ambapo gari za kuzima moto zimefika mahala pa tukio saa mbili baada ya moto kuripuka.
Mwandishi wetu mjini Bujumbura anasema wachuuzi wengi akina mama wamepoteza mali yao yote.
Kumekuwa na ripoti kwamba wakati moto unawaka baadhi ya watu wamepora mali katika soko hilo. 

Waingereza watakiwa waondoke Somaliland Waingereza watakiwa waondoke Somaliland


Uingereza imewashauri wananchi wake waondoke Somaliland kwa sababu za usalama.
Ramani ya Somalia

Wizara ya Mashauri ya Nchi za Nje ya Uingereza inasema kuna tishio maalumu linalowakabili watu kutoka mataifa ya magharibi walioko Somaliland na raia wa Uingereza wanafaa kuondoka haraka.
nafikiriwa kuwa kuna Waingereza wachache tu katika eneo hilo, wengi wao wafanyakazi wa mashirika ya misaada, lakini wengine wenye uraia wa Somalia na Uingereza wanasafiri baina ya Uingereza na Somaliland.
Siku kadha zilizopita, Uingereza na mataifa mengine ya Ulaya yalionya raia wake mjini Banghazi, Libya, kuhusu tishio linalowakabili.

Thursday, January 24, 2013

Jeshi la Mali ladaiwa kuwaua raia

24 Januari, 2013 - Saa 08:23 GMT
Mwanajeshi wa Kifaransa akiwa amesimama karibu na kifaru mjini Niono 20 Januari
Jeshi la Mali limewaua “kiholela watu kadhaa” katika harakati za kujaribu kuteka tena eneo la kaskazini lililoko chini ya mamlaka ya wapiganaji wa Waisilamu. Hii ni kwa mujibu wa kikundi cha kutetea haki za binadamu.
Shirikisho la Kimataifa la Kutetea Haki za Binadamu, FIDH, limesema kwamba watu kadhaa waliuwawa kwa ajili tu walikuwa hawana vitambulisho.
Lakini mwanajeshi mmoja wa Mali alinukuliwa akikanusha madai hayo.
Madai mengine kuhusu mauaji ya kiholela pia yameripotiwa katika maeneo mengine ya magharibi na kati mwa nchi hiyo.
Wanajeshi wa Mali wapiaga doria mjini Diabali 22 Januari
Habari zinazosema kwamba jeshi hilo, ambalo wengi wao ni Waafrika weusi kutoka kusini mwa nchi, wamekuwa wakiwalenga Waarabu na Watuareg kutoka kaskazini, jambo linaloashiria ubaguzi wa rangi katika mapigano hayo, ubaguzi ambao umefichwa na kuwepo kwa vikosi kutoka nchi za magharibi wanaopambana na wanamgambo Kiisilamu, Mark Doyle wa BBC aliyeko Mali alisema.
'Uongo mtupu’
Shirika hilo la kutetea haki lilisema kwamba ni sharti kuwe na uchunguzi huru dhidi ya dhuluma hizo zilizofanywa na wanajeshi wa Mali, na kwamba wote waliotekeleza mauaji hayo wafaa waadhibiwe.
Katika kambi ya kijeshi mjini Sevare, takriban watu saba waliuwawa karibu na kituo cha basi na hospitali, shirika hilo lilisema.
Kuna “habari za kuaminika” kwamba watu wengine 20 waliuawa Sevare, huku miili yao "ikizikwa haraharaka, hususan katika visima. Kuna madai mengine kwamba mauji yangali yanaendelea", shirika hilo lilisema.
Mauaji kama hayo pia yalifanywa katika miji ua Mopti na Niono.
Washirika
Lilizidi kusema kuwa waathiriwa walishtakiwa kwa kuwa na silaha, na kwa kuwa "washirika" wa wanamgambo hao.
Nyumba za makumi ya Watuareg walioko Bamako, mji mkuu wa Mali, zimevamiwa na wanajeshi.
Capt Modibo Traore wa jeshi la Mali alisema kwamba madai hayo "yalikuwa uongo mtupu”, lakini akakataa kufafanua zaidi, shirika la habari la AP liliripoti.
Wakimbizi
Wakati huo huo, Umoja wa Mataifa umesema kwamba raia 7,100 wameshatorokea nchi jirani tangu Jaunuari 10 January ili kuepuka mapigano hayo.
Afisa wa Umoja wa Mataifa Valentin Tapsoba alisema kwamba watu 7,100 walikuwa wametorokea nchi jirani katika majuma mawili yaliyopita. Wengi wao - 4,000 – walitorokea Mauritania, alisema.
Aliongezea kwamba wengine 3,100 walikuwa wamevuka hadi Burkina Faso na Chad, mashariki mwa Mali.
Takriban watu 10,000 wamehamia makambi ya wakimbizi nchini Mali tangu 10 Januari, alisema.
Wakimbizi walioko kambini mjini Sevare
Mzozo huu wa hivi karibuni ulizuka baada ya wanamgambo kuanza kuelekea kusini, wakishambulia miji ya Konna, Diabaly na Douentza iliyoko katikati mwa nchi.
Ufaransa
Ufaransa ilituma wanajeshi wake mnamo 11 Januari ili kukwamisha hatua za wanamgambo hao.
Ilisema kwamba waasi hao, wenye uhusiano na al-Qaeda – na ambao wengine wao si Wamali – walikuwa wametoa tishio kwamba wataigeuza Mali kuwa "nchi ya magaidi".
Maafisa wa Ufaransa wamesema kwamba wanajeshi wao wamewasaidia wanajeshi wa Malia ili kuteka tena miji hiyo mitatu.
Ufaransa inategemea kuipa nchi ya Afrika Magharibi uongozi wa majeshi hayo ya pamoja, idadi ambayo kwa sasa ni 1,000.
 
⬆
Top