ACCRA, Ghana
POLISI nchini Ghana wamemkamata dokta anayehusika na masuala ya oparesheni za kusafisha vizazi (abortion), baada ya kutuhumiwa kumbaka mwanamke aliyefika katika kituo chake kwa ajili ya kusafishwa ujauzito wake.
Daktari huyo Joshua Dran anaaminika kubaka maelfu ya wanawake kutokana na idadi kubwa ya wanawake ambao wamejitokeza hivi sasa wakidai kufanyiwa vitendo hivyo na daktari huyo ambaye huwaomba kufanya ngono ndipo afungue mifereji ya uzazi kwa ajili
ya kusafishwa.
"Kwa upande wake kulikuwa na bei maalum ya maelewano kwa ajili ya utoaji mimba. Zaidi ada yake ilikuwa ni kati ya pesa ya Ghana yenye thamani ya ¢50 na ¢100 ambayo aliichukua kabla ya oparesheni husika.
Kwa wateja wazuri kulikuwa na malipo ya ziada, daktari huyu alihitaji ngono kabla ya kumsafisha mgonjwa, baadhi ya vyombo vya habari nchini Ghana vimeripoti.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo, Dr Joshua Dran amekanusha madai hayo, lakini alishangazwa na video ambayo iliwekwa na wapelelezi wa kesi hiyo iliyomwonyesha yeye akimtendea mgonjwa wake kitendo hicho kabla ya kumtoa mimba katika hospitali yake.
Dran anaendesha klinic ya Universal Mission Clinic iliyopo Madina mjini Accra. Kiongozi mpelelezi katika kesi hiyo Anas Aremeyaw Anas,aliwaambia waandishi wa habari kuwa "tulipokea kesi nyingi kutoka kwa huyu bwana na alikuwa akitoa mimba za wanawake kinyume cha sheria za nchi na suala hilo limepelekea vifo vya watoto wengi pamoja na matatizo ya ugumba na hata wanawake wenyewe kufariki baadaye" alisema Anas.

Post a Comment