Dodoma
MBUNGE wa Tabora Mjini Ismal Aden Rage anatarajia kufikshwa mahakamani wakati wowote kutoka na tuhuma za kushiriki na kumpiga kada wa Chadema wakati wa vurugu zilizotokea kati ya wafuasi wa Chadema na baadhi ya wabunge wa CCM, akiwamo Rage wakati walipokuwa wakigombea mlingoti wa bendera, kitendo kilichosababisha watu watatu kujeruhiwa katika tukio hilo wikiendi iliyopita mjini Dodoma.
Akizungumza na Habarimpya.com mjini Dodoma Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, David Misime amesema kuwa wanaandaa utaratibu wa kumfikisha Mbunge huyo Kortini baada ya jalada la kuhusika katika vurugu hizo na kumpiga kada huyo wa Chadema kukamilika.
Kamanda Misime amesema kuwa baada ya jalada hilo kukamilika litafikishwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), "Ni kweli tumepokea malalamiko ya Chadema na tunaandaa jalada ili kuwasilisha kwa mwanasheria wa Serikali,” alisema Misime.
Kwa upande wake Rage alikanusha kuhusika katika tukio la kumpiga kada huyo na kusema“Sikumpiga. Historia yangu inaonyesha kuwa sijawahi kushiriki vitendo vya vurugu wala mapigano kwa sababu yoyote ile. Mimi siyo mhuni wa kupiga mtu. Nilichofanya ni kumlinda yule kijana asipigwe na wanaCCM waliojaa hasira kwa yeye kuingilia mkutano wetu,” alisema Rage, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Klabu ya Simba.

Post a Comment