Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, kesho atafanya sherehe kubwa ya
kutimiza miaka 91 kwa kuchinja tembo wawili. Sherehe hizo zitafanyika
kwenye mji wa Victoria Falls na zinaandaliwa na chama tawala ZANU-PF
kinataka kukusanya dola za Kimarekani milioni 1 kwa ajili ya sherehe ya
kesho. Wageni wapatao 20,000 wanatarajiwa kuhudhuria. Hata hivyo,
mashirika ya kutetea ulinzi wa wanyama pori yamemkosoa Mugabe, wakisema
haiwezekani akakemea uharamia wakati yeye mwenyewe anaamuru wanyamapori
wachinjwe. Pamoja na hayo baadhi ya raia wa Zimbabwe wanakerwa na uamuzi
wa rais wao kufanya sherehe kubwa kama hiyo, wakati wananchi wake wengi
ni maskini.
credit: DW
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Post a Comment