Maafisa wanne wa polisi na raia
wawili wameuawa baada ya watu wasiojulikana kuvamia kituo cha polisi
mjini Dar es salaam Tanzania.
Shambulizi hilo limetokea katika kituo cha polisi kilichoko Ukonga, viungani mwa jiji kuu la Dar es salaam.Polisi wanasema kuwa wavamizi hao walitekeleza shambulizi hilo la kuvizia usiku wa kuamkia leo.
Waliwafyatulia risasi maafisa wa polisi katika kituo hicho na kuua wanne.
Hadi sasa haijabainika iwapo kuna majeruhi.
Aidha inasemekana kuwa walipora handaki ya kituo hicho na kuiba bunduki 30 za polisi na idadi ya risasi isiyojulikana.
Hakuna aliyekamatwa kufuatia shambulizi hilo japo maafisa wa upelelezi wanaendelea na uchunguzi.
Polisi wanawahutubia waandishi katika kituo hicho.
Hakuna kundi lililokiri kutekeleza shambulizi hilo
credit: ramamedia2010
dah
ReplyDelete