ASkofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam Muadham Policup Kadinari Pengo,kwa pamoja na maaskofu wengine wakichomeka Msalaba katika kaburi la marehemu Padri Evaristus Gabriel Mushi,aliyezikwa jana katika viwanja vya kanisa Katoliki la Kitope, Wilaya ya Kaskazini B Unguja,ambae alifariki Jumapili Iliyopita kwa kupigwa risasi na watu wasiojukanwa.
Rais wa Zanbzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt,Ali Mohamed Shein,(katikati) akiweka shada la mauwa katika kaburi la Marehemu Padri Evaristus Gabriel Mushi,wakati wa mazishi yake yaliyofanyika jana katika viwanja vya kanisa la Kitope, Wilaya ya Kaskazini B Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt,Ali Mohamed Shein,(katikati)akifuatana
na Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Zanzibar Augustino Shao
wakielekea katika Mazishi ya Padri Evaristus Gabriel Mushi,aliyezikwa
katika viwanja vya kanisa la Kitope,Wilaya ya Kaskazini B Unguja.
Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Tanga Antony Banzi, akiongoza sala wakati wa mazishi ya Marehemu
Padri Evaristus Gabriel Mushi,aliyekufa kwa kupigwa risasi Jumapili Iliyopita na kuzikwa leo katika viwanja vya kanisa la Kitope, Wilaya ya kaskazini B Unguja jana.
Padri Evaristus Gabriel Mushi,aliyekufa kwa kupigwa risasi Jumapili Iliyopita na kuzikwa leo katika viwanja vya kanisa la Kitope, Wilaya ya kaskazini B Unguja jana.
Vijana waumini wa Dini ya Kikiristo wakiteremsha jeneza lenye mwili wa marehemu Padri Evaristus Gabriel Mushi,katika kaburi alilozikwa jana katika viwanja vya kanisa la Katoliki la Kitope, Wilaya ya Kaskazini B Unguja, marehemu alifariki kwa kupigwa risasi Jumapili iliyopita na watu wasiojulikanwa.
Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Zanzibar Augustino Shao, akitia udongo katika kaburi la Marehemu Padri
Evaristus Gabriel Mushi,aliyezikwa jana katika viwanja vya kanisa Katoliki la Kitope, Wilaya ya Kaskazini B Unguja.
Evaristus Gabriel Mushi,aliyezikwa jana katika viwanja vya kanisa Katoliki la Kitope, Wilaya ya Kaskazini B Unguja.
Rais wa Zanbzibar na Mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi Dkt,Ali Mohamed Shein, (katikati) akitia udongo katika kaburi la Marehemu Padri Evaristus Gabriel Mushi, wakati wa mazishi yake yaliyofanyika jana katika viwanja vya kanisa la Kitope,Wilaya ya Kaskazini B Unguja.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Emanuel Nchimbi ,akitia udongo katika kaburi la Marehemu Padri Evaristus Gabriel Mushi, wakati wa mazishi yake yaliyofanyika jana katika viwanja vya kanisa la Kitope,Wilaya ya Kaskazini B Unguja.
Vijana waumini wa Dini ya Kikiristo wakiteremsha udongo wakati wa mazishi ya marehemu Padri Evaristus Gabriel Mushi, katika kaburi alilozikwa jana katika viwanja vya kanisa la Katoliki la Kitope, Wilaya ya Kaskazini B Unguja, marehemu alifariki kwa kupigwa risasi Jumapili iliyopita na watu wasiojulikanwa.
Baadhi ya waumini wa kanisa katoliki wakiwa katika mazishi ya marehemu Padri Evaristus Gabriel Mushi, aliyezikwa jana katika viwanja vya kanisa Katoliki la Kitope, Wilaya ya Kaskazini B Unguja.
(Picha zote na Ramadhan Othman, Ikulu-Zanzibar)
---
Na Maelezo Zanzibar
Mamia ya Wananchi wa Zanzibar jana
wameshiriki Mazishi ya Padri Evaristus Mushi aliyeuwawa kwa kupigwa
Risasi na Watu wasiojulikana ambayo yamefanyika katika kijiji cha Kitope
Wilaya ya Kaskazini B, Unguja. Katika mazishi hayo Rais wa Zanzibar
Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamo wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Shariff
Hamad,Viongozi wa Serikali na Vyama vya siasa walihudhuria.
Akitoa salamu za Serikali katika Mazishi
hayo Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mohammed Aboud
Mohammed alisema Serikali imeguswa sana na kifo cha Padri huyo na
kuongeza kuwa itahakikisha waliohusika na tukio la mauji hayo
wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Kwa upande wake Askofu wa Kanisa la
Anglikacana Michael hafidh amewataka Waamini wa dini ya kikristo kuwa
watulivu bila kulipiza kisasi bali waiachie Serikali kufanya kazi yake
ili kuwabaini waliopoteza Uhai wa Marehemu huyo.
Awali Mazishi hayo yalitanguliwa na Misa
takatifu ya kumuombea Marehemu iliyoendeshwa na Askofu Mkuu wa Kanisa
Katoliki Jimbo kuu la Dar es Salaam Muadhama Policarp Kadinali Pengo
katika Kanisa la Minara Miwili Mjini Zanzibar.
Padri Mushi alifariki dunia Februari 17
baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana wakati akielekea Kanisani
kuendesha Misa ya Asubuhi katika Kigangwe cha Mtakatifu Teresia eneo la
Beit El Raas mjini Unguja Enzi za uhai wake Padri Mushi alikuwa Msomi wa
Shahada ya Uzamivu ya Elimu ya Ushauri nasaha aliyoipata nchini
Marekani ambapo umauti ulimkuta akiwa anaelekea kuendesha Ibada ya
Jumapili ya kwanza ya Kwarezma.
Padri Evarist Mushi wa Kanisa la Minara
Miwili mjini Zanzibar alizaliwa June 15, 1957 Mkoa wa Kilimanjaro akiwa
ni mtoto wa nne katika familia ya watoto sita ya Mzee Mushi.
Post a Comment