Stori: George Kayala
MSANII wa sanaa ya maigizo Bongo, Ummy Wenslaus ‘Dokii’ juzikati ameifungukia ishu yake ya ulokole na kujishughulisha na mambo mbalimbali ambayo baadhi ya walokole hawayapendi.

Continued after the jump ....
Akichonga na ‘kachala’ wa Funguka na Risasi hivi karibuni jijini Dar,
Dokii alisema anatambua yeye ni mlokole na anampenda Mungu kuliko watu
wanavyofikiria.
Fuatana nami katika aya zifuatazo ili kujua kile alichofunguka:
Funguka: Bwana Yesu asifiwe Dokii.
Dokii: Ameeen, habari za siku nyingi!
Funguka: Nzuri sana. Ebwana! Siku za nyuma ilisemekana uliokoka na kuachana na matendo maovu na ukafanikiwa kutoa albamu moja ya nyimbo za injili lakini nasikia umepotoka, kulikoni?
Dokii: Nani kasema nimekengeuka. Mimi ni mlokole safi hata Mungu anajua hilo. Hata mimi nasikia watu wanasema nimeachana na wokovu lakini hawajui suala la wokovu ni la mtu binafsi na Mungu wake.
Funguka: Unahisi kwa nini wanasema umeachana na wokovu?
Dokii: Nafikiri kwa sababu ya kuona nimerejea katika masuala ya sanaa ambayo ndiyo yalinifanya nijulikane mpaka leo hii. Watu wengine huwa wananishangaa kuona nimesuka aina fulani ya mtindo ambao huwa hawaupendi.
Funguka: Inasemekana umekuwa ukienda kwenye majukwaa ya kumbi za burudani na kufanya mambo ambayo ni chukizo mbele za Mungu likiwemo suala la kukata mauno mbele za watu na kuonekana kama huna wokovu ndani yako. Je, ni kweli?
Dokii: Siyo kweli. Mimi huwa siwaelewi watu wanaojiita walokole kwa kufuatilia maisha ya mtu. Hata maandiko yanasema asiyefanya kazi na asile. Sasa mimi nikifanya kazi ya sanaa naonekana ni mtenda dhambi.
Wangapi
ambao wanafanya mambo ambayo ni machukizo mbele za Mungu na hawasemi
chochote? Nimesoma sana Biblia sijaona sehemu inapomuelekeza mtu kazi ya
kufanya bali imesema asiyefanya kazi na asile. Ninachojua mimi nafanya
kazi ambayo ni halali hata Mungu anaitambua, wanaosema mimi nimekengeuka
wananikosea heshima.Fuatana nami katika aya zifuatazo ili kujua kile alichofunguka:
Funguka: Bwana Yesu asifiwe Dokii.
Dokii: Ameeen, habari za siku nyingi!
Funguka: Nzuri sana. Ebwana! Siku za nyuma ilisemekana uliokoka na kuachana na matendo maovu na ukafanikiwa kutoa albamu moja ya nyimbo za injili lakini nasikia umepotoka, kulikoni?
Dokii: Nani kasema nimekengeuka. Mimi ni mlokole safi hata Mungu anajua hilo. Hata mimi nasikia watu wanasema nimeachana na wokovu lakini hawajui suala la wokovu ni la mtu binafsi na Mungu wake.
Funguka: Unahisi kwa nini wanasema umeachana na wokovu?
Dokii: Nafikiri kwa sababu ya kuona nimerejea katika masuala ya sanaa ambayo ndiyo yalinifanya nijulikane mpaka leo hii. Watu wengine huwa wananishangaa kuona nimesuka aina fulani ya mtindo ambao huwa hawaupendi.
Funguka: Inasemekana umekuwa ukienda kwenye majukwaa ya kumbi za burudani na kufanya mambo ambayo ni chukizo mbele za Mungu likiwemo suala la kukata mauno mbele za watu na kuonekana kama huna wokovu ndani yako. Je, ni kweli?
Dokii: Siyo kweli. Mimi huwa siwaelewi watu wanaojiita walokole kwa kufuatilia maisha ya mtu. Hata maandiko yanasema asiyefanya kazi na asile. Sasa mimi nikifanya kazi ya sanaa naonekana ni mtenda dhambi.
Funguka: Kwa nini uliamua kuachana na uimbaji wa nyimbo za injili ukaanza kuimba nyimbo nyingine?
Dokii: Mimi bado ni mwimbaji wa nyimbo za injili na mpaka sasa ninaimba katika kwaya moja maeneo ya Mwananyamala, ukifika hapo ndiyo watakwambia kama kweli mimi nimeacha wokovu.
Funguka: Unaimba katika kwaya gani?
Dokii: Subiri kwanza nipokee simu hii kwani ni muhimu sana, naweza kukosa dili la fedha sasa hivi. Samahani kwa hilo naomba usijisikie vibaya.
(Baada ya muda) naomba mazungumzo yetu tuyasitishe kwanza nimepigiwa simu ya muhimu sana kuna mtu nilikuwa na miadi naye tangu jana kwa ajili ya safari ya kwenda Dodoma, naomba uniruhusu niondoke wakati mwingine tutaongea.
Funguka: Poa nitakucheki wiki ijayo endelea na mishemishe zao.
Post a Comment