Games

LATEST UPDATES

Saturday, July 18, 2015

NDUGU YAKE DIAMOND AZUIWA KUINGIA NYUMBANI KWA ZARI

Rose na rafiki yake wakigonga getini kwa Diamond.
Mrembo aliyedai ni dada wa hiyari wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ aliyejitambulisha kwa jina moja la Rose akijiita wifi wa mwandani wa jamaa huyo, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, hivi karibuni ameumia kupita maelezo baada ya kuzuiwa kuingia nyumbani kwa mastaa hao, Ijumaa lina mkanda mzima.
Rose ambaye ni ‘msichana wa mujini’ alijikuta akitiliwa ngumu na mlinzi nyumbani kwa Diamond maeneo ya Tegeta-Madale, Dar ambapo alikwenda kumuona Zari baada ya kusikia yupo Bongo.
IMG_0020Mlinzi akiwakatalia kuingia ndani.
Kwa mujibu wa Rose, kabla ya Diamond kuwa na uhusiano na Zari walikuwa wapo vizuri lakini baada ya kuwa na mama kijacho huyo, hajawahi kumuona na amekuwa akitamani waonane laivu bila mafanikio.
“Zari ni wifi yangu kwa Diamond (bila kufafanua uwifi kivipi). Pia napenda sana kazi za Diamond lakini tangu waanzishe uhusiano kila ninavyojitahidi niwaone inakuwa ngumu. Ningepata msaada wa kuwaona ningefurahi.
“Nilijaribu kuomba msaada kwa kaka mmoja ambaye ni rafiki wa Diamond lakini akaniambia Zari akiwepo pale nyumbani kwa Diamond hasa kipindi hiki ambacho ni mjamzito, ni ngumu mtu yeyote kuingia,” alisema mrembo huyo.
Ijumaa laamua kumpeleka

IMG_0028Baada ya kushindikana kumuona wifi yake amabaye ni ‘Zari’, Rose aliamua kurudi nyumbani.
Katika kuhakikisha kama alichokuwa akikisema kina ukweli, mmoja wa waandishi wa gazeti hili juzi Jumatano aliamua kumsindikiza Rose hadi nyumbani kwa staa huyo lakini katika hali ya kushangaza, mlinzi binafsi aliyekutwa aliweka ngumu kumfungulia mlango mdada huyo.
“Wewe kama unasema Diamond ni kaka yako na Zari ni wifi yako, ungewapigia simu kabla ya kuja, siwezi kuwafungulia geti,” alisema mlinzi huyo.
Rose: Lakini kaka ungenisaidia tu nikaingia ndani, Diamond akiniona hawezi kunizuia.
Mlinzi: Haiwezekani, tena naomba muondoke.
Kufuatia kuwekewa ngumu huko, mdada huyo aliondoka eneo hilo huku akiwa amenyong’onyea ambapo wakati hayo yote yakiendelea, mmoja wa mapaparazi wetu alikuwa akipiga picha kwa simu ya mkononi.
Diamond-Platnumz-na-ZariDiamond na Zari.
Kumbe ulinzi mkali
Baada ya dada huyo kutokubaliwa kuingia ndani ya nyumba ya Diamond licha ya kudai ni wifi wa Zari, Ijumaa lilizungumza na baadhi ya watu wanaoishi eneo hilo ambapo walisema ni ngumu sana kupenya kuingia ndani ya mjengo huo.
“Pale bwana wapo wengi wanakuja na kudai ni ndugu wa Diamond lakini wanaishia nje na kuondoka, bila taarifa mlinzi hawezi kukufungulia geti, kwa hiyo kuzuiwa kwa huyo anayedai ni wifi wa Zari siyo ishu,” alisema kijana mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Shebe.
DIAMOND ANAMJUA?
Kama kawaida yake ya kutoa ujumbe upande mmoja na kupeleka upande wa pili ili kupata mzani, ‘kijumbe’ wa gazeti hili alimtafuta Diamond kwa mahewa akiwa kwenye ‘pipa’ kuelekea nchini Afrika Kusini ‘Sauzi’ ambapo alijibu kwa kifupi: “Nimekwambia simjui huyo dada.”
SIYO ROSE PEKEE
Mbali na Queen Darleen na Esma ambao ni dada zake wa ukweli wanaofahamika, wapo wasichana wengine kibao mjini ambao nao hudai ni dada zake wa hiari ambapo ukimwacha Rose pia yumo Halima Haroun ‘Kimwana’ ambaye hata Zari anamuita wifi licha ya kwamba hana undugu na Diamond.
DIAMOND KULAMBA TUZO
Wakati hayo yakiendelea, wikiendi hii Diamond anatarajiwa kulamba tuzo zinazofanyika Sauzi za MTV Music (Mama) baada ya kuteuliwa kuwania Vipengele vya Msanii Bora wa Kiume Afrika, Mtumbuizaji Bora wa Kiume Afrika na Wimbo Bora wa Kushirikiana Afrika.
KILA LA HERI DIAMOND
Dawati la Ijumaa linamtakia Diamond kila la heri ili ailetee heshima Tanzania katika anga la muziki wa Bongo Fleva. -Mhariri.globalpublishers
Share This :

Post a Comment

 

Top