Mtangazaji maarufu nchini, Maimartha Jesse.
Gladness Mallya
MTANGAZAJI maarufu
ambaye siku chache zilizopita amejiunga na Azam Tv, Maimartha Jesse
amewafikisha wafuasi wa Wema Sepetu wanaojulikana kwa jina la ‘Team
(Timu) Wema’ kwa mwanasheria wake kutokana na kuendelea na tabia yao ya
kumtukana kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii.
Baada ya hivi karibuni gazeti ndugu na
hili kuripoti habari juu ya mwanadada huyo kumshtaki Wema na wafuasi
wake kwa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum, Dar, Suleiman Kova bado
wameendelea kumshushia matusi ya nguoni hivyo kulazimika kwenda kwa
mwanasheria wake anayejulikana kwa jina la Mrema ambapo analifanyia kazi
suala hilo.
“Nimechoka na ninaapa kwamba nitakula
nao sahani moja kwani mpaka sasa nimeshagundua kuwa kuna mmoja yupo
Malaysia na mwingine India huku waliobaki wako hapahapa Dar hivyo
mwanasheria wangu anaendelea kulifanyia kazi hilo kwani wanaendelea
kunitukana kila kukicha,” alisema Maimartha.
source: globalPublishers
Post a Comment