Mkutano wa viongozi wote 28 wa nchi za ulaya uliopangwa kufanyika leo kujadili suala la deni la Ugiriki umefutiliwa mbali.
Mkutano
huo unafutilia mbali wakati mawaziri wa fedha wa nchi za ulaya
wanakutana kwa mazungumzo kujaribu kuafikia makubaliano kuhusu msaada
kwa nchi ya ugiriki.Akitangaza kufutiliwa mkutano huo rais wa baraza la ulaya Donald Tusk alisema kuwa mpango wa mkutano huo utakuwepo hadi mazungumzo kuhusu ugiriki yatakapokamilika.
Mwandishi mmoja mjini Brussels anasema kuwa kuna sababu moja ya kufutiliwa mbali mkutanio ambayo ni kuangazia suala la kuiwezesha Ugiriki kusalia kwenye mataifa yanayotumia sarafu ya euro.
Yamkini mawaziri wa fedha wanaendelea na mazungumzo magumu, kutafuta muafaka kuhusu msaada ambao Ugiriki inafaa kupewa.
Mawaziri hao walivunja kikao jana usiku na wanaendelea tena leo.
Slovakia ni kati ya nchi zinazoonesha wasiwasi kuhusu mapendekezo ya karibuni ya serikali ya Ugiriki.
Waziri wa Fedha wa Slovakia, Peter Kazimir, alipoulizwa na waandishi wa habari, alionesha wazi hasira zake.
Wakati wa saa tisa za mazungumzo mjini Brussels siku ya Jumamosi Euclid Tsakalotos alishindwa kuzishawishi nchi zingine za ulaya kuwa Ugiriki ina mipango mizuri ya kumaliza tatizo lake la deni.
Serikali ya Ugiriki inaomba mkopo mpya wa karibu euro bilioni 70.
Ujerumani imekuwa ikidai kuwa Ugiriki itaondoka kwa muda kwenye nchi zinazotumia safaru ya euro hatua ambayo inapingwa na Ufaransa na baadhi ya nchi za ulaya zinazo ihurumia Ugiriki.
Mawaziri hao wanatarajia kuwa na mpango kabla ya mkutano wa viongozi wa nchi za ulaya ambao utafanyika baadye hii leo.
Post a Comment