Kama
alivyowashangaza wengi pale alipojitokeza kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa na
CCM kuwania urais Mei 29 mwaka huu,2015, ndivyo Dk John Magufuli
alivyowashangaza tena jana Julai 10,2015 kufikia hatua hii ya tano bora.
Magufuli ,
alipochukua fomu alisema tu kuwa kipaumbelea chake ni kutekeleza ilani ya
uchagzi ya CCM.
Hata katika
safari yake ya kusaka wadhamini mikoani, mbunge huyo wa Chato alikwenda kimya
kimya, bila mbwembwe, ahadi wala kukusanya mashabiki.
Bila hiyo
ndiyo siri yake ya ushindi, alihofia kukatwa mapema kwa kukiuka masharti ya
chama, kama ilivyowatokea wengine.
Hata kabla
hajachukua fomu, Dk Magufuli hakuwahi kutangaza nia yake ya kuwania urais, hadi
alipoibuka ghafla na papo hapo akapenya hadi hatua hii muhimu, hadi
alipolidokeza gazeti hili mjini Dodoma.
“Swali hili
nimeulizwa mara nyingi. Mara zote nimekataa kulijibu kwa sababu katika chama
chetu (CCM) kuna utaratibu wake wa namna ya kuomba nafasi ya uongozi. Muda
ulikuwa haujawadia.
Lakini
utakumbuka wiki hii hapa hapa Dodoma, vikao vya juu vya chama chetu vimetoa
ratiba kwa wanaotaka kuwania nafasi mbalimbali kujitokeza. Kwa maana hiyo sasa
niko huru kujibu swali lako kwa kusema rasmi ‘nitagombea urais’.
Alipojaribu
mara ya pili baada ya jimbo kutengwa na kuanzishwa Chato akaibuka mshindi, sasa
wanajivunia kuwa na shule nyingi za sekondari zikiwamo wa Muungano, Meghji na
Chato na nyingine zikiwa na kidato cha tano na sita, suala ambalo Francis
anasema lisingewezekana bila Dk Magufuli.
“Nafanya
hivyo kwa sababu naamini ninazo sifa za kuchagua na kuchaguliwa kama mwanachama
wa CCM kwa nafasi yoyote inayojitokeza kulingana na Katiba ya chama chetu na
pia Katiba ya nchi,” alisema Dk Magufuli.
Pamoja na
kutokuwa na papara za kutangaza nia wala kuanza kupitapita kwa wanachama
kutafuta kuungwa mkono, Dk Magufuli alikuwa vinywani mwa watu wengi, ndani na
nje ya CCM, wakisema akiteuliwa anaweza kuleta ushindani dhidi ya upinzani.
Waziri huyo
wa muda mrefu na maarufu kwa kumbukumbu na kukariri takwimu mbalimbali, kila
wizara anayokwenda inageuka maarufu na kuanza kusikika, lakini kazi kubwa
inayomweka kwenye mwanga wa kisiasa nap engine hata kumfikisha katika hatua hii
ni wizara ya Ujenzi na hasa usimamizi wa ujenzi wa miundombinu.
Dk Magufuli
alizaliwa katika Kijiji cha Rubambangwe kilichopo Wilaya ya Chato mkoani Geita,
ndipo unapoweza kukutana na wananchi ambao wanafahamu maisha yake ya ujana na
hatua alizopita hadi hadi hatua ya leo.
Kuna
simulizi za kusisimua kuhusu maisha ya Magufuli ambaye wananchi wengi wa jimbo
lake wanamtumia kama alama ya ushindi, akihusishwa na mafanikio ya kujitenga
kutoka Wilaya ya Biharamulo hadi wakapata jimbo na hatimaye Wilaya.
Alivyoachishwa
kazi
Kama
ilivyowahi kuelezwa na gazeti hili, wakazi wa Chato wanaamini kuwa Dk Magufuli
hakuwa na ndoto za kuwa mwanasiasa mpaka aliposhawishiwa na wazee kugombea
ubunge baada ya kuona wamekuwa wanyonge kwa muda mrefu.
Mzee Emmanuel
Francis anayakumbuka maisha ya ujana ya Magufuli, ‘’Wazee tulikaa na kumuona
huyu ndiye msomi wa kiwango cha juu anayeweza kutukomboa tulikuwa tunamfuatilia
tangu akiwa mwalimu shule ya sekondari Sengerema hata alipokuwa mkemia kwenye
shirika la pamba,” alibainisha Francis.
Anasema
Magufuli hakuwakatisha tama, alikubali kujitosa kugombea ubunge akipambana na
Phares Kabuye (sasa marehemu) ingawa matokeo hayakukidhi kiu yao, japokuwa
mgombea mwenyewe aliyakubali.
Tukio la
Magufuli kumshika na kumpongeza mshindani wake liliwashangaza na kumuona kama
kijana asiye na kinyongo.
KIlichomponza
hata hakina maana, wanasema hata uvaaji wake wa miwani ulimpunguzia kiasi
fulani cha kura baada ya baadhi yao kuamini kuwa miwani ni kielelezo cha usomi
na hivyo asingekuwa kiongozi wa kukimbiliwa.
‘’Wasukuma
tuna kasumba ya kupigiwa magoti, baadhi ya wananchi walipomuona ni kijana
anayependa kuvaa miwani walisema huyu ndiye atatusahau kabisa,” anabainisha
Francis.
Tetesi za
urais
Wanakijiji
wenzake wanakiri kuvuma kwa jina la mbunge wao na kutajwa miongoni mwa
waliokuwa wanataka kuwania urais katika.
Francis
anasema hana wasiwasi na kutajwa kwa jina la mbunge wake miongoni mwa wanataka
uongozi wa nchi kwa kuwa amepata uzoefu mkubwa kupitia wizara alizoongoza
katika awamu tofauti.
“Amepita
katika wizara nyingi bila kuwa na tuhuma za ubadhilifu kama ilivyotokea kwa
mawaziri wengine, alionyesha uadilifu na kila wizara aliyoongoza ilionekana
kuwa imara na yenye mafanikio,” alisema Francis.
Tangu awali,
mzee huyo na wenzake walibainisha kuwa wanatamani mbunge huyo achukue fomu ya
kugombea nafasi ya urais, huku akiamini kuwa anaweza kuungwa mkono na wananchi
wengi kutokana na historia yake ya kuwatumikia kwa uadilifu.
Hata hivyo,
wasiwasi wa wengi ni kuwa waadilifu wa aina yake ni vigumu kupata nafasi hadi
kufikia kiwango cha kupendekezwa kuwania uongozi wa nchi kwa kuwa kuna makundi
hayawapendi.
Mchunga
ng’ombe
Familia ya
Magufuli ambaye ni baba yake na John ilikuwa ya wafugaji, hivyo watoto
waliozaliwa katika kaya hiyo kwa vyovyote vile wasingeweza kulikwepa jukumu la
kuchunga ng’ombe.
Hata wakati
wa likizo wananchi walizoea kumuona John akifanya kazi za kawaida za nyumbani
ikiwa ni pamoja na kuchunga ng’ombe na kukamua maziwa wakati wa likizo.
“Baba yake
alikuwa na mifugo mingi na hakuwa mtu wa kujikweza, wakati wa likizo tulizoea
kumuona John akifanya kazi za nyumbani hata kwenda shambani kulima na kukamua
maziwa,” alisema mkazi wa kijiji hicho.
Mkazi
mwingine, Maritha Rufunga ana kumbukumbu tofauti kuhusu maisha ya ujana wa
mbunge huyo na hata hajasahau wakati mbunge huyo kwa sasa alipoanza safari yake
kielimu kwa kujikwaa.
“Hakuwa na
majivuno na hata alipomaliza shule na kushindwa kuchaguliwa baba yake alikuwa
amekataa asiendelee na masomo, lakini kuna mwalimu wake alikwenda kumtetea kwa
baba yake ili akarudie shule,” alisema Maritha Rufunga.
Post a Comment