Tuesday, July 14, 2015
KUMEKUCHA: NAIBU KATIBU MKUU CUF TAIFA MHE MAGDALENA SAKAYA KUELEZA NINI KILICHOENDELEA NDANI YA UKAWA.
Author enoMedia on 5:48:00 PM in - Comments : 0
Mhe SAKAYA kuzungumza na wandishi wa habari pamoja na wanachama wote wa Cuf sababu na kwanini chama chake kilichojengwa kwa misingi ya HAKI SAWA KWA WOTE kinashidwa kwenenda na misingi ya DHURUMA.
Huwezi ukasema uko kwenye mashirikiano wkt mwingine anajigeuza BIG FISH na kutaka 70% ya MAJIMBO na hapo hapo anataka mgombea wa urais atoke kwenye chama chake.
Huwezi kwernda na chama ambacho kilimwita LOWASSA mwizi, Fisadi, na leo kinafanya harakati na mazungumzo ili awe mgombea kupitia UKAWA huku ni kukosa SERIOUSNESS ya kiuongozi.
Huwezi kusafiri na chama kinachofanya ushawishi kwa Mkurugenzi wetu JUSSA ili awe mgombea mwenza wa LOWASSA kupitia chadema wkt Lowassa tumekuwa tukimtangaza kuwa na fisadi mzoefu.
Huwezi kwenda na chama kinachotaka tuchague mgombea wa UKAWA bila sifa wala vigezo bali kwa HOJA moja tu anakubalika wkt huyo mgombea akifanikiwa kushinda atakuwa na kazi ya kuwaongoza watanzania.
Huwezi kusafiri na chama kilicho tayari vyama vingine vyote VIFE lakini wao wafanikiwe hakuna VIGEZO vyovyote vya kumpata mgombea zaidi ya hisia binafsi za kwao kuwa mgombea wao anakubalika hata kama hana SIFA awe yeye tu.
TUMEGOMA HATUENDI KWANZA MISINGI YETU YA HAKI SAWA KWA WOTE HAIJAZINGATIWA KATIKA MGAWANYO .
Ni mkutano muhimu sana na wandishi wa habari wanachama wote mnakaribishwa
ASIBAKI MTU NYUMBANI TWENDE NA LIPUMBA MWAKA WA MAAMUZI
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Post a Comment