Stori: Gordon Kalulunga, Mbeya
Uchawi! Uchawi! Uchawi! Mwanamke ambaye ni mke wa mtu, aliyetajwa kwa jina moja la Zai, mkazi wa Mtaa wa Ilolo, Kata ya Manga jijini hapa amenusurika kuuawa baada ya kuponzwa na tuhuma za mambo ya ulozi au ushirikina.
Tukio hilo lililoshuhudiwa na Amani lilijiri maeneo hayo mwanzoni mwa
wiki hii ambapo wananchi takriban 200 waliitisha mkutano, wakitaka
kujichukulia sheria mkononi kwa kumpiga na kumchomea moto nyumba
mtuhumiwa huyo waliyedai kuchoshwa na maovu anayowafanyia.…
Stori: Gordon Kalulunga, MbeyaUchawi! Uchawi! Uchawi! Mwanamke ambaye ni mke wa mtu, aliyetajwa kwa jina moja la Zai, mkazi wa Mtaa wa Ilolo, Kata ya Manga jijini hapa amenusurika kuuawa baada ya kuponzwa na tuhuma za mambo ya ulozi au ushirikina.
Tukio hilo lililoshuhudiwa na Amani lilijiri maeneo hayo mwanzoni mwa wiki hii ambapo wananchi takriban 200 waliitisha mkutano, wakitaka kujichukulia sheria mkononi kwa kumpiga na kumchomea moto nyumba mtuhumiwa huyo waliyedai kuchoshwa na maovu anayowafanyia.
Walidai kuwa mwanamke huyo akimgusa mjamzito huwa mimba inaharibika huku wanafunzi wanaotoka katika mtaa huo wakifika shuleni hushindwa kuona, yote hayo yakihusishwa na mwanamke huyo.
Walisema mwanamke huyo anatuhumiwa kujihusisha na matukio ya kishirikina tangu ahamie mtaani miaka mitatu iliyopita ambapo walisema wakazi hao walimuonya mapema kuhusu tabia hiyo baada ya kufuatilia historia ya maeneo aliyowahi kuishi.
Kwa upande wake mumewe, Rubea (49), alikanusha mkewe kuhusika na ushirikina huku akiwatupia lawama wananchi hao kuwa wanaendekeza udini na hawapendi mtu wa dini nyingine tofauti na ya kwao (haikutajwa ni dini gani).
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Mtaa wa Ilolo Kati, Ngambi Kulaba, wananchi hao walikuwa wakimtuhumu yeye kuwa anamlinda mwanamke huyo lakini baada ya kuona raia wamepagawa na kutaka kujichukulia sheria mkononi, ilimlazimu kuwataarifu polisi ambao walifika na kukuta bonge la mtiti kisha kumuokoa mwanamke huyo na kuondoka naye kwa usalama wake.
Post a Comment