Games

LATEST UPDATES

Thursday, February 14, 2013

RAY NA STEVE NYERERE WAKOSANA KWA PENZI LA MAINDA


MASTAA wawili wenye majina makubwa ndani ya Bongo Movies, Vincent Kigosi ‘Ray’ na Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ wanadaiwa kuwa kwenye bifu zito kisa kikielezwa kuwa ni mwigizaji , Ruth Suka ‘Mainda’,

Kwa mujibu wa vyanzo makini vilivyo karibu na mastaa hao, hofu imetanda kwamba huenda wawili hao wakazama kwenye ugomvi kama ule wa Ray na marehemu Steven Kanumba.

 
“Ugomvi wa Ray na marehemu ulikuwa mdogo ila ulikuzwa na alipofariki dunia Kanumba kuliibuka mambo mengi sana, naomba marafiki wa dhati wa wawili hawa wakae nao ili kuweka mambo sawa,” ’ alisema mwigizaji mmoja.

Inadaiwa kuwa chanzo cha yote ni pale Steve Nyerere alipoanzisha kampuni ya kazi zake za sanaa akimshirikisha Mainda, jambo linalosemekana kumkera Ray aliyekuwa akifanya kazi na mwigizaji huyo wa kike chini ya Kampuni ya RJ Production.

 
“Kuna wakati eti Ray huwa hapendi kumuona mtu akiwa karibu na Mainda, mara nyingi huwa anakuwa na wivu kwa kuwa anahisi kuna kitu zaidi ya kazi,” kilisema chanzo kingine na kusisitiza kuwa Ray alimpiga ‘stop’ Mainda kushirikiana na Steve Nyerere huku suala la wivu wa kimapenzi likitajwa.


Ilidaiwa kuwa kabla ya mtafaruku huo, Steve Nyerere na Ray walikuwa ni maswahiba lakini sasa wamegeuka chui na paka na katika kutafuta ‘sosi’ ya yote hayo, ndipo Mainda akatajwa.


Vyanzo hivyo vilifunguka kuwa hali hiyo ilizua tafrani kubwa kwa kuwa tayari filamu ya Steve Nyerere (jina kapuni) ilikuwa imeanza kurekodiwa.



Baada ya kupata taarifa hizi, mwandishi aliwatafuta wahusika, wa kwanza alikuwa Steve Nyerere, alipoulizwa kuhusiana na hilo alikiri kutokea kwa ishu hiyo.


“Ni kweli mimi na Ray ni chui na paka lakini sitaweza kukwambia sababu ya ugomvi wetu kwa kuwa nitaibua mambo mengi sana, kipindi hiki nipo katika kubadilisha maisha yangu,” alisema Steve Nyerere.


Ray alipotafutwa kwa simu ya kiganjani hakupatikana na hata alipofuatwa ofisini kwake Sinza-Mori, Dar hakuwepo.


Kwa upande wake Mainda, simu yake iliita bila kupokelewa hivyo jitihada za kuwapata wawili hao ili nao wafunguke ya moyoni mwao zinaendelea.
Share This :

Post a Comment

 

Top