MTWARA WAMBANA PINDA, WAMPINGA
Author
Unknown
on
7:58:00 AM
in
-
Moja ya picha ya tukio la Maandamano zidi ya madai ya Kupinga gesi kuitoka Mtwara kwa bomba hadi Dar es Salaam
LICHA ya Waziri Mkuu,
Mizengo Pinda kufichua siri akiwa Dodoma kuwa amebaini kuwa kuna mpasuko
mkubwa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), mkoani Mtwara na harakati za
kisiasa ni sababu zilizochochea mgogoro huo wa madai ya gesi, baadhi ya
wananchi mkoani hapa bado hawajaridhika hivyo wameyakataa maelezo yake.
Baadhi
ya wananchi waliomsikiliza waziri mkuu walisema hawakubaliani na
maelezo yake na Taasisi ya Shura ya Maimamu Mtwara imesema kwamba
haijaridhishwa na majibu yasiyo na mashiko ya Pinda katika hoja nzito na
kwamba bado serikali haijaupatia suluhu mgogoro huo.
“Wana Mtwara
tunahitaji ‘powerplant’, mashine za kufua umeme pamoja na hiyo ya
kuchakata gesi iwe Mtwara… katika eneo hilo hatujaridhika,” msemaji wa
shura hiyo, Sheikh Abubakar Mbuki alisema.
“Waziri Mkuu asituambie tu
gharama za kutandaza nyaya ni kubwa kuliko bomba la gesi akaishia hapo.
Atuambie gharama hizo ni kiasi gani? Mbona gharama za bomba zipo wazi,
kwa nini hizi za nyaya hazisemwi?” alihoji Sheikh Mbuki.
Naye
Mwenyekiti wa Vijana wa Chama cha Wananchi (CUF) Taifa, Katani Katani
alikuwa na haya ya kusema: “Tunachokataa sisi wana Mtwara ni kusafirisha
gesi kwa njia ya bomba, tunataka mashine zinazojengwa Kinyerezi
zihamishiwe Mtwara.”
Alisema kutokana na kutopatikana kwa ufumbuzi wa
madai hayo, bado wananchi wa Mtwara wataendelea kupinga mradi huo na
hali itakuwa tete.
Post a Comment