Games

LATEST UPDATES

Friday, March 8, 2013

BAADA YA YOUNG TUSO KUIMBA NDIO MZEE REMIX BILA YA IDHINI YA PROF. JAY......PROF JAY AELEZA JINSI ALIVYO CHUKULIA KITENDO HICHO

Wimbo wa Ndio Mzee ulioimbwa na Prof. Jay ni maarufu sana hasa kwa watu tunaofatilia Bongo Fleva na ni moja KATI ya nyimbo zilizofanya vizuri sana kipindi hicho.
Hivi majuzi msanii chipukizi kutoka Temeke anayejulikana kama Young Tuso aliamua kuurudia wimbo huo ila si kwa verse zilezile NOH ni kwa mistari yake ye mwenyewe ila issue ilikuja pale alipofanya kitendo hicho bila ya kumuhusisha mhusika wa song hilo ambaye ni Wa Mitulinga ze prof jizzee.
Katika interview aliyofanya wiki hii na clouds Fm Young Tuso alitumia fursa hiyo kuomba msamaha na kujitetea kua alimtafuta Jay ili umwomba lakini hakufanikiwa kuonana naye hivo akaamua kufanya kama suprise kwa Jay, Baada ya hapo alitafutwa Jay kwa njia ya simu na kufunguka kua ye alisikia tu kua kuna dogo amerudia wimbo huo ila yeye bado hata hajausikia kabisa wimbo huo.
Alipoulizwa kachukuliaje kitendo hicho bila wenge wala nini akasema ni kawaida tu hasa anafurahi kuona wasanii wapya wanarudia nyimbo za zamani ni kufanya kitu kinachoitwa KEEPING GOOD MUSIC ALIVE
Share This :

1 comment :

  1. Hongereni blog ni nzuri ila wekeni mobile view itakua poa zaid mIA MIA WADAU

    ReplyDelete

 

Top