Baada ya jana Diamond Platnumz kufunguka kwa undani jinsi
anavyochukizwa na kitendo cha mwanamuziki mwenzie Abubakar Katwila aka Q-Chief
kumsema anatembelea nyota yake, Q-Chief ameamua kumjibu Diamond
Katika kipindi cha XXL cha Clouds FM jana, Diamond
alisema,
“mimi sipendezewi na anvyowaambia watu kuwa mimi namloga, kwa nini
nisitembelee nyota ya watu kama akina Omary, akina Ben Pol. Alumbane na wakubwa
wenzie akina Dully Sykes, mimi sitaki, namheshimu abishane na wakubwa wenzie,
mimi mdogo aniache na wadogo wenzangu.
”
Naye Q_chief alijimjibu kwa kusema hivi
“Sijui wakati anajibu hayo maswali alikuwa kwenye hali
gani, sijui alikuwa amekasirika, sijui alikuwa 'out of mood' sijui alikuwa
okay, lakini 'all in all' najua kila mtu ana uhuru wa kuongea kile
anachojisikia na hajawekea mipaka, as long as kina-msatisfy yeye na
kinawafurahisha wengine kwenye umma.
Mimi watu wangu wamenichukulia positive hili jambo baada
ya kusikikiliza walinirekodia nikasikiliza lakini 'am not a big fan of
superstition so' siamini hivyo vitu lakini kitu ambacho naweza kusema huu najua
ni mchezo mchafu na acha niucheze kwa hisia kwa sababu sijui huko mbele ni kitu
gani kitakuja kunisaidia katika maisha na kunyamaza pia wakubwa wanasema ni
ustaarabu. He is a good kid, I love his music, he is doing good.”
Pia aliongeza kwa kusema hivi
“Ningependa awepo kwenye hii show aangalie kwa sababu
mimi pia nimekuwa nikihudhuria na nimeshawahi kufanya show ya Diamonds are
Forever naye aliniita kwa mapenzi yake and with open-hearted I did a good
show,”
Show hiyo itafanyika February 24 ndani ya New Maisha Club
Post a Comment