Games

LATEST UPDATES

Friday, August 21, 2015

MAKANYA AJITOSA KUWANIA UDIWANI KATA YA MUGANGO

Katika kipindi hiki ambacho kinaonesha kuwa vijana wanayataka mabadiliko. Kijana mwenzao ndg Omary Musa Makanya ajitosa kuwania udiwani kata ya mugango. Akiongea na ripota wetu mapema wiki hii alithibitisha jambo hilo na akiomba sapoti kubwa kutoka kwenu ili
 kufanikisha kaingia kwake mjengoni na kutatua changamoto zinazokabili kata hio

 wasifu wake: amemaliza elimu ya msingi huko Kisumu Kenya katika shule ya msingi Kanyamedha ilioko kisumu kisha alijiunga na elimu ya upili ktk shule ya sekondari kisumu day ambapo baada ya kuhitimu 2004 alirudi nchini Tanzania lakini hakuishia hapo kwani mwaka 2006 alirejea tena kisumu kufanya diploma in electrical installation kwa miaka 3. Sasa anagombea nafasi ya udiwani kupitia tiketi ya chama cha ACT WAZALENDO, mwaka wake wa kuzaliwa ni 6.11.1984
 Anaomba kura ZENU za ndio wakazi wote wa Mugango, Naomba tumuunge mkono kwa mabadiliko ndio sisi, wewe na yule na tunaamini uzalendo wa kweli ni ule unaojali na kuweka maslahi ya Taifa mbele. Asanteni



Share This :

Post a Comment

 

Top