NYOTA wa nyimbo za Injili Bongo, Rose
Muhando amesema hakuna jambo jema alilojifunza tangu abadili dini kutoka
kwenye Uislamu na kuwa Mkristo zaidi ya ‘ugaidi’ wa kiroho mbaya na
sasa anaangalia namna ya kurudi katika imani yake ya kwanza.
Muimbaji maarufu wa nyimbo za Injili nchini, Rose Muhando.
Akizungumza na Amani hivi karibuni, Rose
alisema hana furaha katika maisha ya Ukristo tofauti na alivyokuwa
akielezwa wakati akihubiriwa kuokoka.
Pia Rose alikwenda mbali zaidi kwa
kuwarushia madongo baadhi ya wachungaji kwa kumhukumu kwa maneno ya
walimwengu bila kutumia hekima za kidini.
“Wakati nahubiriwa kuokoka, niliambiwa nitakutana na upendo lakini matokeo yake nimekuwa mtu wa ‘kupigwa mashuti’ tu.
“Mfano, mtu anakualika kwenye tamasha,
kwa bahati mbaya unashindwa kufika na unampa taarifa lakini kesho yake
unasikia umetapeli, wameshindwa kuona hata jema moja kwangu? Nafikiria
kurudi kwenye dini yangu, naamini nitapata faraja,” alisema Rose.
Mwimbaji huyo amekuwa akikumbwa na
skendo ya utapeli ambapo hudaiwa kupokea fedha kwa ajili ya kutumbuiza
kwenye matamasha ya dini halafu kuingia mitini.
credit: ukurasawahabari blog
Post a Comment