Games

LATEST UPDATES

Monday, July 13, 2015

NAKUPENDA MAMA heart emoticon 01

Sad Story:NAKUPENDA MAMA heart emoticon
Mtunzi;Emmanuel G Sendama
MsAkaTongE OriJinO
Mobile/WhatsApp 0688857280

"Nakupenda sana mama yangu.Nakupenda hata kama wengine wanakuchukia.
Nawachukia Maishani mwangu wote wanaokuchukia...!!
Ni nani asiyekuwa na Mama katika Ulimwengu huu.?
Hata kama mama yake ameshatangulia mbele za haki,lakini lazima alizaliwa na mwanamke kama wewe.
Je.! Hao wanaokuchukia walizaliwa na Baba zao??
Mbona wanakuwa na Roho za Kikatili namna hii...!

Walikuona hufanani na mama zao kwa sababu wewe ni KICHAA.
Ndio,wewe ni kichaa lakini haibadilishi ukweli kuwa wewe ndiye Mama yangu mzazi.
Mwanamke uliyenipenda japo hukuwa na Akili timamu.
Ulionekana mjinga ila kwangu ulikuwa na Akili nyingi kuliko mama zao.
Ulikula Vichafu jalalani ila ulijua kuwa mimi nahitaji ziwa lako kwa ajili ya Shibe yangu.
Hukutaka kutengana nami hata dakika moja tu,
na mda wote ulinipakata mikononi mwako.
Walioona mama zao wana akili, waliwaacha mikononi mwa wafanyakazi wa ndani kwa kisingizio wako busy na kazi.
Wewe mama yangu ulikuwa tofauti sana.
Ulikuwa busy na mimi mwanao....

Mama uliyetembea Uchi maishani mwako,
ila mimi ulikumbuka kunifunika na Matambara machafu uliyoyaokota jalalani.
Hukuwa na uwezo wa kuninunulia nguo,ila ULINIJALI.
Ni upendo wa aina gani uliokuwa nao mama...!!
Mwanamke waliyekupa majina yote mabaya Duniani;
Walikuita Chizi,
wakakuita Kichaa,mwehu na mwisho kabisa wakakuita MALAYA....!!
Yaani mama yangu unaitwa Malaya.??
Umalaya ni tabia ya mwanamke kuuza mwili wake kwa shida au starehe binafsi.
Mama yangu hukuwa Malaya.
Ungepata wapi mda wa kujiuza wakati ulishinda Majalalani ukitafuta mabaki ya vyakula vyilivyotupwa....!
Hukupata hata mda wa kujipodoa ili kujiweka safi kama wanawake wa Kileo.
Akili zako zilikuwa pungufu mama yangu...

Ulitembea uchi bila kujua thamani yako mbele ya watu.
Lakini WANAUME wasiokuwa na Ubinadamu walifurahia kuona maungo yako.
Wakakuvizia na kujua unapolala;
Usiku wa manane wakakufuata jalalani ulipopageuza kitanda.
Wakapandwa na Pepo mbaya.
Wakajawa na Roho za kishetani.
Wanaume mawakala wa Ibirisi wenye Tamaa ya Ngono,
WAKAKUBAKA MAMA YANGU....!!

Wanaume zaidi ya mmoja wakaweka Uchafu wao maungoni mwako.
Uchafu uliogeuka Baraka na kusababisha Mimba yangu...!
Mama ukawa Mjamzito baada ya kubakwa.
Ukageuka GUMZO mtaani pote ulipoonekana.
Watu wakashangaa Mwanamke Kichaa kupata mimba...!!
Wengi wakacheka na kusema hata nyie vichaa mna Ny*ge....
Wakakutolea maneno ya Kejeli na dharau.
Hukuwajali mama yangu,
ukaendelea na Maisha yako huku mie nikiwa sijitambui tumboni mwako.

Laiti wangejua maumivu uliyokuwa nayo moyoni mwako.
Maumivu ya kubakwa na wanaume wabaya usiowajua.
Maumivu yaliyokupa jina jipya.
Jina baya ambalo halifurahii mwanamke yoyote yule DUNIANI.
Ukaitwa MALAYA.
Hata mie mwanao nalichukia sana jina hili..!!
Ila wewe Mama yangu uliitwa jina hili popote ulipopita.
"KICHAA MALAYA..."

Wewe sio Malaya mama yangu.
MALAYA NI WANAUME WALIOKUBAKA....!!
Ndio; wao ni Malaya maana wana Tamaa ya ngono.
Hawakujali hali yako,
shida ulizokuwa nazo,
na upungufu wa Akili uliokusumbua.
Wao wakakuongezea tatizo jingine; Wakakubaka...!
Haikuwa kazi ngumu kwao kukuvua nguo zako,maana zilikuwa tayari zimeshavulika.
Nguo zilizoisha na kubaki kama Tambara la Deki,zilikuwa zimefunika mwili wako...
Siku hii zilivuliwa na wanaume hawa WAKATILI.

Hawakujali tena kama ulikuwa MCHAFU.
Mchana walikuona UNANUKA ila Usiku wakakuona UNANUKIA.
Pepo mbaya wa Ngono hakuwaruhusu kufikiria yote hayo...!!
Mama yangu UKALIA,
lakini Hukusikilizwa.
*Inamaana walikosa hata CHANGUDOA wa kufanya naye huu Upumbavu wao.??
Samahani kwa kutukana ila naomba niseme ukweli wangu....
"NAWACHUKIA WANAUME WOTE DUNIANI..."

Wanaume wako radhi kumtelekeza Mwanamke na mtoto waliyemzalisha.
Wanaume ni watu Wabaya sana.
Siku hii Usiku walimbaka mama yangu...!!
JIULIZE; ingekuwaje leo hii wewe ungetelekezwa na Baba yako au Ungezaliwa ukasikia MAMA YAKO ALIBAKWA kukupata wewe..!
Hapo ndipo mtajua MAUMIVU NILIYONAYO...

*Itaendeleaa
Share This :

Post a Comment

 

Top