Sad story:NAKUPENDA MAMA heart emoticon
Mtunzi;Emmanuel G Sendama
MsAkaTongE OriJinO
Mobile/WhatsApp
0688857280
Ilipoishia.....
JIULIZE; Ingekuwaje leo hii wewe ungetelekezwa na Baba yako.?
Au ungezaliwa ukasikia kuwa MAMA YAKO ALIBAKWA kukupata wewe....!!
Hapo ndipo utajua MAUMIVU NILIYONAYO....
*Endelea...
Pamoja na kuwa haukuwa na Akili timamu, lakini ulitambua sio haki wewe KUBAKWA.
Ukalia mama yangu.
Ukapiga kelele za kuomba msaada,
Lakini wote waliokusikia wakapuuzia kwa kujua wewe ni Kichaa.
Mama ukakosa mtu wa kukusaidia.
Wanaume wenye misuli imara wakakukamata kwa nguvu,
na mmoja baada ya mwingine akakidhi haja zake.
Wakakupa Ujauzito wangu.
Miongoni mwa wanaume hao ndipo yupo Baba yangu...!!
BABA KATILI, ninayemchukia kuliko SHETANI...!
Mwanaume aliyekutelekeza na tumbo lako ulilohangaika nalo Mitaani.
Mwanaume ambaye hata yeye hajijui kuwa ndiye Baba yangu mzazi...!
Atajijua vipi wakati walikubaka wengi.?
Baba yangu ni mmoja tu kati yao.
NASIKITIKA kuwa mtoto wa Mbakaji.
ULAANIWE BABA YANGU......!!
Sitakusamehe kamwe.
***
Uliteseka mama yangu.
Ulihangaika nami miezi yote tisa niliyokuwa tumboni mwako.
Mchana na usiku,
Hatimaye UKANIZAA kwa Shida usiku jalalani.
Hakuwepo yeyote wa Kukusaidia...!!
Nikarithi maisha ya UCHOKORAA tangu nazaliwa.
Maisha ya kula mabaki kama Mbwa...!!
Tangu nilipokuwa mdogo,ulinilinda na hatari zote mbaya.
Hukuruhusu mtu yeyote aniguse, na ulikuwa upo tayari kukabiliana naye kunusuru Maisha yangu.
Ulinipenda sana Mama.
Hukufikiria hata siku moja KUNITUPA.
Japo ulikuwa CHIZI ila kwangu ulionekana JINIAZI..!
Nawashangaa sana Wanawake wanaowatupa Watoto wao.
Tena wao huonekana wana Akili Timamu kuliko wewe Kichaa.
Wao ni Vichaa wa ndani kwa ndani.
Utamtupaje mwanao Aliyemwaga damu yako wakati wa Kumzaa.
NAWALAANI MAISHANI MWANGU....!!
Mpaka ninakua nipo mikoni mwako.
Chini ya uangalizi wako imara...!!
Kwanini Nisikupende Mama yangu.??
NAKUPENDA SANA MAMA...
Ila leo hii NALIA...!!
Naumia sana nikikumbuka siku niliyokukuta katika hali ile.
Hali mbaya iliyomsisimua kila mtu aliyekuwepo.
Kila aliyekutazama alilia au kushika mikono kichwani mwake.
Walikuonea huruma....!!
HURUMA YA KINAFIKI...!???
Ni Huruma ipi waliyonayo ikiwa walikutazama kama Sinema.
Mama yangu upo chini ukivuja Damu kama Bomba lililotelekezwa na DAWASCO.
UMEGONGWA GARI na MWANAUME mlevi aliyekimbia baada ya Ajali kutokea.
Umati mkubwa wa watu wamekuzunguka,
lakini hakuna hata mmoja aliyefikiria kukusaidia.
Nilifika katikati ya Umati ule na kukukuta katika hali mbaya sana.
Mama ulikuwa ukitapatapa kupigania Roho yako.
Nilijitahidi kukuinua lakini nilishindwa...!!
Nilikuwa bado mdogo na ulikuwa mzito kwangu...
Mama Kichaa;
Siku hii ulitamka maneno ninayoyakumbuka na kuyaandika mda huu.
Ulinisimulia HISTORIA YA MAISHA YANGU YOTE...!!
Ulinisihi nimtafute Baba yangu,
maana wewe hutaweza tena kuwa nami Duniani.
Nimtafute Baba aliyekubaka, akishirikiana na wanaume wengine.
Mi nitamjua vipi Mama...!??
Mama ulinitazama na kusema.....
"NA..NA..NAK..NAKUPEEE..ND A....SANAAAAA EMMA mwanangu...!
Chukua mkufu huu ili ubaki kama Kumbukumbu Maishani mwakooooo....!"
Baada ya kusema hivyo MAMA ULIKATA ROHO...!!
Ulifia mikononi mwangu, watu wamenizunguka wakitutazama bila msaada.
Baada ya dakika 5 tu tangu kufa kwako,
walikuja Polisi na kunitoa kwa nguvu mwilini mwako.
Wakakuchukua na kukupeleka walikokujua wao...!
Niliwafuata Kuona walipokupeleka...!
MAKABURINI...
Mama, Ulizikwa KIKATILI na Manispaa ya Jiji.
Hakuna uchunguzi wowote uliofanyiwa.
Hakuna hata mmoja aliyejitolea japo kunua SANDA au JENEZA la kukuhifadhi katika Nyumba yako ya Milele.
MAMA YANGU ULIZIKWA NDANI YA GUNIA KAMA MBWA..!!
Hapana Mamaaaaa...!!
Hii sio haki mama yangu.....
Uliwakosea nini watu hawa.??
Wameumbwa na Mungu yupi asiyewafunza HURUMA....!
Ni bora nami Nikufuate mama yangu...
Sioni Faida ya kubaki kwenye hii DUNIA YA MAKATILI....
MAJITU MABAYA yasiyokuwa na Huruma hata punje....!
Lakini;
Sipaswi kujiua Mama,
ili Nibaki Duniani KUKUOMBEA na KUOMBOLEZA KIFO CHAKO.
Nibaki KUPALILIA KABURI LAKO.....!!
Acha niseme maneno haya nawe...
"NAKUPENDA SANA MAMA YANGU;
PUMZIKA KWA AMANI.
TUTAONANA TENA MBINGUNI....! Amen"
Nilimaliza kuongea na MKUFU huu alioniacha Mama yangu kipenzi.
DAIMA NILIUTHAMINI na kuuona kama mama yangu Mzazi,
aliyebaki nami kupitia mkufu huu wenye picha yake kwa Ndani.
MACHOZI yalikuwa yamelowanisha mashavu yangu na Macho yalikuwa mekundu kwa Kulia.
Nilipiga magoti na KUMUOMBEA MAMA YANGU...!
REST IN PEACE MOMY:
I will LOVE U Forever
(Ntakupenda Daima)
***MWISHO***
NB:Hii ni hadithi fupi niliyoitunga ili kuwathamini Mama zetu.
Kama yupo mwambie leo NAKUPENDA MAMA..!
Akiwa mbali mpigie simu umwambie maneno haya.
Kama ameshatangulia Mbele za haki sema
REST IN PEACE MOMY:
NTAKUPENDA DAIMA.
Asanteni.
By MsAkaTongE OG

"NA..NA..NAK..NAKUPEEE..ND

i love you mama
ReplyDelete