Annastazia Fredy,Mwanza
WAZIRI Mkuu aliyejiuzuru Edward Lowassa Bbunge wa Monduli amesema
yeye sio fisadi wala tajiri wa mali bali ni tajiri wa watu kama baadhi
ya watu wasemavyo.
Akizungumza katika kongamano la maombi ya akina mama duniani
yaliyofanyika katika kanisa la Anglican tawi la Nyamanoro jijini Mwanza
Lowassa alisema kwamba watu wengi wanamuuta fisadi kimakosa kwa sababu
yeye si fisadi bali yeye ni tajiri.
“Mimi sio fisadi wala tajiri wa mali bali mimi ni tajiri wa watu niko
kwa ajili ya kusaidia watu sio kama watu wanidhaniavyo kuwa mimi ni
tajiri wa mali” alisema Lowassa.
Aidha aliiomba serikali kurudisha mabilioni ya rais Kikwete ili
kusaidia wananwake vijijini waliopo kwenye vikundi vya vikoba ili waweze
kujikwamua kiuchumi na kukuza uchumi wa Taifa.
Usemi huo umekuja baada ya Naibu Katibu wa Umoja wa Wanawake wa
Kikiristo Manispaa ya Ilemela Paulina Gasabile wakati alipokuwa akisoma
risala yake kwa mgeni rasimi ambapo alisema kuwa wanavikundi 40 wenye
wanachama 1200 huku wakiwa na hisa yenye milioni 18.
Katibu huyo alisema kuwa vikundi hivyo vinasaidia wanachama kupata
pesa na kuwakopesha na mpaka hivi sasa wanachama 68 wameshapata kiasi
cha sh. 2million kwa ajili ya kuhakikisha wanawake wanajikwamua kiuchumi
.
Hata hivyo kufuatia tukio hilo Lowassa alichukua jukumu la kufanya
harambee na kufanikisha kiasi cha sh.39 millioni ili kutunisha mfuko wa
umoja wa wanawake wa kikristo jijini mwanza kupitia vikoba wanasonga
mbele na kuondoka na tatizo la umasikini.
Post a Comment