2 Machi, 2013 - Saa 03:56 GMT
Kiongozi mmoja mkuu
wa kundi la wapiganaji la al-Qaeda ameuawa nchini Mali. Taarifa hizi
zimethibitishwa na Rais wa Chad, Idriss Deby
Alisema kuwa majeshi ya nchi yalimuua Abdelhamid
Abou Zeid, wakati wa makabiliano yaliyotokea katika eneo moja la
vijijini nchini Mali.
Anasemekana kuwa wa pili kwa ngazi ya uongizi katika kundi hilo ambalo linapigana na majeshi ya kigeni nchini Mali.
Raia huo wa Algeria anatuhumiwa kwa mauaji ya
mateka wawili kutoka nchi za magharibi Edwin Dyer raia muingereza mwaka
2009 Michel Germaneau raia wa ufaransa mwaka uliofuata.
Mwandishi wa BBC Thomas Fessy anasema kuwa ikiwa
wataweza kuthibitisha kifo hicho, maswali bila shaka yataibuka kuhusu
mateka wa Ufaransa wanaoaminika kuwa walikuwa mikononi mwa Abou Zeid.
Mwezi Januari, Ufaransa ilituma wanajeshi 3,500,
Kaskazini mwa Mali, kwa lengo la kuwafurusha wanamgambo wa kiisilamu
waliokuwa wameteka sehemu ya jangwa la Sahara.
Chad ni mojawapo ya nchi nyingi za Afrika ambazo zinaunga mkono harakati za jeshi la Ufaransa nchini Mali.
Post a Comment