Games

LATEST UPDATES

Tuesday, February 12, 2013

SUGU AKERWA NA 2030 YA ROMA




 Msanii wa kwanza kufanya album hapa Bongo na kwa sasa ni mbunge wa Mbeya mjini kupitia tiketi ya CHADEMA, Joseph Mbilinyi a.k.a  Mr II na wengi hupenda kumuita Sugu ameonyesha wazi kukerwa na ambao ameuimba   ROMA katika ngoma yake ya 2030, Sugu  alichodai ROMA ana kurupuka na hajui anachokifanya.

Akizungumza katika kipindi cha TV wiki iliyopita Sugu amesema kuwa msanii huyo anapaswa kuijua misingi ya hip hop na pia Sugu amemuonya na kumtaka roma awe muangalifu na anachokiandika na kukitowa kwa jamii na sio kukurupuka kama mtu aliyestuliwa toka usingizini.

Sugu amesema yeye ni mfuasi wa hip hop hivyo ukitaka kuwa mwana hip hop lazima uzame ndani sana ili ukiandika kitu uwe na uhakika nacho na si kufanya kama Roma anavyofanya.Namtahadharisha bwana mdogo awe muangalifu na anachokiandika na si kukurupuka hip hop ina misingi yake na ni lazima uzame ndani sana maana hip hop ni maisha na ukweli mtupu, pia aelewe hip hop ni sauti ya kumkombowa mnyonge sasa unapoimba mambo ambayo huna uhakika nayo haipendezi maana utakuwa hujaisaidia jamii husika alisema sugu. 

Katika wimbo  huo wa 2030 kuna kipande kina sema pesa ndio imemaliza vita yaRuge na Sugu kitu ambacho kimeonyesha kumkera Sugu na kusema kuwaRoma anakurupuka na kuandika asichokijua maana kwa mstari huo tu umefanya niaamini kila achoandika hana anachokijua maana mstari huu unanihusu na hakuna ukweli juu ya alichokiimba.

Sugu amemtaka Roma kusikiliza nyimbo walizoimba kaka zake ili zimuongoze katika sanaa yake amesema asikize nyimbo kama za profesa jay,afande sele,solo thang atagunduwa kuwa zilikuwa ni harakati za uhakika mfano mdogo amesema asikilize miss Tanzania ya Solo Thang atajua anachomaanisha.


  Roma alipotafutwa kujua amejisikiaje baada ya mheshimiwa kuchukizwa na wimbo wake Roma alisema Sugu ni kaka yake na anaamini kama kuna baya atamuita na atamrekebisha.

Share This :

Post a Comment

 

Top