UONGOZI wa
klabu ya Simba unatarajiwa kwenda nchini Uingereza kwa ajili ya kukutana na
uongozi wa timu ya Sunderland inayoshiriki ligi kuu ya huko.
Aidha, Simba
imemshukuru Rais wa Tanzania Jakata Mrisho Kikwete ambaye alimkutanisha mwenyekiti wa Simba,
Aden Rage na mwenyekiti wa Sunderland, Ellis Short ambaye alikuja nchini.
Ofisa
habari wa Simba Ezekiel Kamwaga amesema leo kwamba hatua ya uongozi wa
Simba kwenda huko inafuatia hatua nzuri ya mazungumzo
ya ushirikiano baina ya pande hizo mbili.
“Kwa kweli
tunamshukuru sana Rais Kikwete kwa kumkutanisha mwenyekiti wetu Rage na Short
na ndipo mambo haya mazuri yakajitokeza,”alisema
Alisema ni
matarajio yao klabu ya Simba itapiga hatua kubwa kupitia ushirikiano na timu
hiyo kongwe nchini Uingereza kwani tayari wameshaanza kukubaliana baadhi ya
mambo ikiwemo uendelezaji wa soka la vijana.
Kamwaga
aliongeza kuwa uongozi wa Simba utakapokuwa nchini Uingereza pamoja na
kushuhudia baadhi ya mechi za timu hiyo, pia utapata fursa ya kubadilishana
uzoefu wa kiuongozi na wenyeji wao.
Post a Comment