Taarifa za msiba wa baba yake mzazi alizipata alhamisi iliyopita akiwa bado yuko nchini Uingereza ambako alikwenda kufanya show toka december 2012.
Baada ya kupata taarifa ilibidi afanye utaratibu wa kupanga safari kurudi nyumbani ili amzike baba yake lakini wakati huohuo siku chache nyuma alikua amepeleka hati yake ya kusafiria Home Office ili aongezewe muda wa miezi mitatu kuendelea kukaa Uuingereza ambako alipata dili pia alikua na mipango ya kufanya video mpya kabla ya kurudi home.
Alishughulikia ticket mchana huohuo alipopata taarifa na akafanikiwa ila tatizo likawa ni kupata documents za kusafiria ili awahi kuja kumzika baba yake siku inayofata ambayo ni ijumaa.
Namkariri Sumalee akisema “niliambiwa we kata ticket ila documents za kusafiria tutapiga simu mtu aende kuchukua ubalozi wa Tanzania U.K ila kuna jamaa pale ubalozini anaitwa Sylvester Ambukile nikaongea nae kwenye simu nikajitambulisha nikamwambia nimefiwa naomba travel documents nikazike, hakutaka kunielewa kabisa yani ndio kwanza ananiambia hatuwezi kukupa kithibitisho kwa sababu passport yako ipo sio kwamba imepotea, wakati huo ilikua ni saa nane mchana na ndege niliyokata ticket inaondoka saa moja usiku”
“Tumewapigia wenzake ubalozini ndio wakaniambia huyu huyo ndio anahusika, dakika za mwisho mwisho ndio tukampata balozi wa Tanzania U.K akasema mbona hiyo inawezekana ila haiwezekani kutoa travel documents bila kupata jina la mtu kuulizia kule home office kama jina lako lipo kweli manake kuna wengine wanafanya makosa wanatafutwa na askari wanataka document ili wakimbie nchi lakini wewe ulitakiwa kumkabidhi jina lako ili aulizie home Office, wakati huo muda ulikua umepita tayari ilikua saa kumi na mbili na nusu ofisi zimeshafungwa” – Sumalee
Mbali na hayo Sumalee amesema “ningefanikiwa kusafiri Alhamisi ningewahi kuzika kabisa lakini kibinaadamu huyu jamaa Sylvester Ambukile nitamlaumu mpaka kufa kwa sababu siwezi kusahau hili tukio kwa sababu ni kitu ambacho kilikua kinawezekana, na sio mimi tu amepigiwa na watu hata 15 wa hapa London kila mtu anamwambia swala langu lakini jamaa alikua anasema siwezi, sitaki na sitaweza, hataki kuelezea hataki kufanya chochote"
Post a Comment