Games

LATEST UPDATES

Monday, February 25, 2013

RAY ADHOHOFIKA ATIA HOFU NDUGU NA JAMAA

MWIGIZAJI Vincent Kigosi ‘Ray’ amezua hofu kwa ndugu, jamaa, marafiki na mashabiki wake baada ya kukongoroka ghafla akihisiwa anaumwa,
Vincent Kigosi ‘Ray’ alivyo kwa sasa.

Wiki kadhaa zilizopita paparazi wetu alishtuka alipomuona Ray kwenye ‘bethidei’ ya mwigizaji sistaduu Yobnesh Yusuph ‘Batuli’ ndani ya Hoteli ya Shamoll iliyopo Sinza ya Lion, Dar akiwa amekongoroka na kuibua maswali kwa wahudhuriaji.
Akiwa ukumbini hapo, minong’ono ilienea kuwa Ray alionekana kukondeana katika kipindi kifupi huku baadhi ya watu wakisikika wakiulizana kulikoni kwani alikuwa meza moja na bonge la mtu, Jacob Steven ‘JB’ hivyo kumfanya kuonekana mdogo mno.

Akiwa kwenye Viwanja vya Leaders, Kinondoni, Dar wiki iliyopita, Ray aliibua mshtuko kwa mara nyingine hadi jamaa mmoja anayedhaniwa kutokuwa vizuri kichwani kumfuata na kumuwakia akimuuliza kwa hasira kuwa kulikoni akondeana kiasi hicho.

Kwa mara nyingine, Ray alizua hofu alipohudhuria kwenye uzinduzi wa ofisi ya Wema Sepetu uliofanyika maeneo ya Kinondoni, Dar ambapo alipoingia watu walipigwa butwaa wakimtazama na wengine kumuonea huruma wakidhani anaumwa.

Kwa nyakati tofauti, wanahabari wetu walizungumza na Ray ambaye alitoa majibu ya kukinzana na kuzidi kutia shaka.
Ray alimwambia mmoja wa waandishi wetu kuwa kilichosababisha akongoroke kiasi hicho ni mazoezi makali anayofanya ili kupunguza unene.
Katika majibu mengine kwa mwandishi wetu mwingine, Ray alidai kuwa anafanya ‘dayati’ ikielezwa kuwa ikishafika saa 11:00 jioni ndiyo mwisho wake wa kula msosi lengo likiwa ni kupunguza mwili uliokuwa umefumuka.
Kama mtu alimuona Ray kwenye Matamasha ya Serengeti Fiesta mwishoni mwa mwaka jana, akikutana naye lazima amtazame mara mbilimbili hivyo Ijumaa Wikienda lipo mzigoni kutafuta undani wa madai kuwa huenda staa huyo mkubwa anaumwa kufuatia majibu
tofauti aliyoyatoa.

CHANZO:Ijumaa Wikienda
Share This :

Post a Comment

 

Top