Jackline Patrick juzi Jumatano alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam na kusomewa shitaka la kumjeruhi kwa chupa kichwani msichana aliyetajwa kwa jina la Hafsa Sasya.
Akisoma shitaka hilo, mbele ya mahakama, Mwendesha Mashitaka mahakamani hapo Silvester Shirikale alisema mshitakiwa anashtakiwa kwa kosa la kumjeruhi vibaya mlalamikaji huyo.
Alisema: “Mnamo Januari 26, mwaka huu maeneo ya Kinondoni jijini Dar es Salaam ndani Hoteli ya Element Lounge mshitakiwa alimpiga kwa chupa kichwani mwanamke mmoja aitwaye Hafsa Sasya na kumjeruhi vibaya.”
Baada ya kusomwa shitaka hilo mbele ya hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo Edna Makabwa, mrembo huyo aliulizwa kama ni kweli au si kweli alitenda kosa hilo ambapo alikana shitaka.
Hakimu aliiahirisha kesi hiyo hadi Machi 13, mwaka huu itakapotajwa tena ambapo alimwambia mshitakiwa kuwa dhamana iko wazi kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili wenye bondi za shilingi 800,000 kila mmoja.
Post a Comment