Fredwaa anayejulikana kwa vituko na utani mwingi awapo studio amehamia kituo cha radio cha Times FM 100.5 cha jijini Dar es Salaam.
Mtangazaji huyo ambaye ni kipenzi cha wengi leo kupitia Facebook ameandika: Amka nasi ndani ya Times FM 100. 5 Sunrise kuanzia saa kumi na mbili asubuhi hadi saa tatu asubuhi , Fully Force Fadhili , Samira na Fredwaa . Let dem know ! …wanaharakati wa asubuhi tuko moto kama pasi.”
Habari hiyo imepokelewa kwa hisia tofauti na mashabiki wake wa mikoani ambako Times FM haisikiki.
Khamis Tembo Colins: Times iko mitaa ya Kawe Dar kaka,mimi mwenyewe amenishangaza saana kwa sababu sikuwahi fikiri siku 1 atachomoka RFA lakini ndio maisha au siyo!!!
Biogas Kwa Maisha Bora: Aiiii…. jmn, RFA kwisha sasa. Mbona wakali wote wanatoka huko? Kaka Fredwaa, je Mama (Rahabu Fred) nae wapi jmn? Kila la kheri kaka, chapa kazi, ila tatizo haipatikani mikoa mingi. Aaaah… tutakukosa sana jmn kaka. “Regger, Raggar Power” kwisha RFA.
Selemani Tambwe II: Hadi Fredwaa umehama rfa na kukimbilia dsm. Karibu proudly African 100.5 fm. Sema umehamia ktk Redio yenye coverage ndogo tofauti na rfa. Sema rfa hakuna ubunifu ndio maana iko static miaka mia 8.
Fredwaa amewapoza mashabiki wake kwa kuwaambia, “Very sorry guyz its all about life tu ! Mungu atubariki daima.
Fredwaa si mtangazaji wa kwanza kuacha kazi Radio Free Afrika siku za hivi karibuni. Ndani ya mwaka mmoja kituo hicho cha radio kilichopo chini ya kampuni Sahara Communications, kimepoteza watangazaji zaidi ya nane wakiwemo Sandu Mpanda aka Kidboy, Fredrick Bundala aka Skywalker, Sam Kiama, Deo Kaji Makomba, Rahab Fred (mke wa Fredwaa) na wengine na hivyo kukiacha taabani.
Post a Comment