Games

LATEST UPDATES

Thursday, February 21, 2013

MAMBO YA WANAWAKE.



Kundi la wake za watu walikuwa
kwenye semina kuhusu namna
ya kuishi kwa upendo katika
ndoa. Muwezeshaji akauliza,
wangapi wanawapenda waume
zao? Wote wakanyoosha mikono.
Akauliza tena, ‘Mara ya mwisho
umemwambia mumeo
nakupenda lini?. Majibu
mbalimbali yalitolewa, Wengine
wakisema Leo, wengine Jana,
wengine hawakumbuki. Kisha
akawaambia, kila mtu achukue
simu yake halafu amtumie
mumewe text yenye maneno.
NAKUPENDA MPENZI, kisha
wabadilishane simu.
Wakaambiwa kila moja asome
majibu kwenye simu aliyoshika,
majibu yalikuwa kama ifuatavyo;

Simu 1- Samahani nani
mwenzangu?
Simu 2- He Mama Joji unaumwa?
Simu 3- Nami pia daima
Simu 4- Nini tena umeshagonga
gari?
Simu 5- Sijakuelewa una maana
gani
Simu 7- Umefanya nini tena? Leo
sitakusamehe
Simu 8-Chukua taim yako
Simu 9-?!?
Simu 10- Acha kuzunguka
unataka shilingi ngapi?
Simu 11 – Hivi naota?
Simu 12 – Kwa kweli leo
usiponieleza hii mesej ulikuwa
unampelekea nani atakufa mtu
shenzi mkubwa
Simu 13 – Nilishakwambia
usirudie kunywa pombe au
ntakuacha naona umechoka
kuishi na mimi

Unaweza ku SHARE kwa wenzako kama umeipenda hii..

Chief...
Share This :

Post a Comment

 

Top