Na Gladness Mallya
MSANII mkongwe kwenye filamu Bongo, Fatuma Makongoro ‘Bi Mwenda’ amepata pigo la kufiwa na mumewe anayejulikana kwa jina la Salum Mbegu.
Akizungumza kwa huzuni, Bi Mwenda alisema mumewe aliugua kwa muda mfupi ambapo Februari 14, mwaka huu alipelekwa katika Hospitali ya Amana ambapo aligundulika kuwa na tatizo la moyo kupanuka, akarudishwa nyumbani na siku iliyofuata (Februari 15) alifariki dunia.
Mipango ya mazishi ilitarajiwa kufanyika Jumamosi iliyopita nyumbani kwa marehemu, Kitunda, Dar. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi, Amina.

Post a Comment