Games

LATEST UPDATES

Thursday, January 24, 2013

MAHUSIANO HAYA BHANA

Usitaje jina plz. Ndugu, Nahitaji ushauri kwa jamaa zangu. Mimi ni mtoto wa pili na mwisho kwa mama angu, pia ni mtoto wa sita kwa baba angu. Baba angu alimuoa mama angu mwaka 1984 baada ya kuachana na mke aliekua nae. Baadae mwaka 1990 mimi nilizaliwa. Pindi baba angu anaachana na huyo mama, tayari watoto watano walikua wameshazaliwa hivyo waliachwa pale nyumbani na mama angu ndo akachukua jukumu la kuwalea mpaka ukubwa wao. Kwa kifupi, kuanzia huo mwaka, 1984 ndugu zangu hao hawakuwahi ishi na mama yao. Basi, siku ndo hizo, ilipofika mwaka 2003 migogoro ilianza tokea katika familia kitu kilichopeleakea hao ndugu zangu kuanza kunichukia. Walianza ongea hata maneno ya kunitakia mabaya mojawapo ni kuomba nifeli mtihani wa darasa la saba. Lakini nashukuru mungu, nilifaulu na kuchaguliwa kujiunga na shule ya kata iliyopo karibu na nyumbani kwetu. Mwenendo wangu kimasomo ulikua mzuri kiukweli. Walivyokua wakisikia mambo mazuri juu yangu, kiukweli walikua wakitoa kauli za kukatisha tamaa. Kipindi hicho, kaka zangu wawili walikua wameshaanza kazi za Ualimu sehemu tofauti tofauti. Kiukweli, hawakuwahi kunisaidia hata senti moja katika shule ingawa baba angu alikua akitoa pesa ya karo(namshukuru kwa hilo) tu. Maswala ya tuition na vitabu ilikua ni juu yangu. Basi, huku wakiombea mimi nifeli katika masomo yangu, cha ajabu nilipomaliza form 4, nilipata moja ya matokeo mazuri sana shuleni na hata wilayani kwetu ukilinganisha na shule niliyokua nasoma. Nilichaguliwa kujiunga na kidato cha tano mwaka 2009 mchepuo wa PCB. Kipindi niko form five, moja ya kaka zangu nilimbip kwa kutumia namba mpya nikiwa shuleni. Basi alivyokuja kupiga, aliuliza nani? Kabla sijajibu akawa ameshaijua sauti yangu na kutaja jina langu. Alivyotaja tu jina akakata simu na hakunipigia tena mpaka leo. Kaka mwingine nae hata hakuwahi kunipigia simu wala kujua shule ilikua ikiendeleaje. Basi, nikawa nimemaliza kidato cha sita mwaka 2011, nilifaulu vizuri sana pia na kufanikiwa kujiunga na chuo kikuu kuchukua shahada ya udakitari. Sasa nipo mwaka wa pili katika moja ya vyuo vya udakitari hapa nchini. Basi, ningependa kuomba ushauri wenu ndugu, kama either niendelee kuwatafuta hawa ndugu zangu ama niachane nao ingawa wao hawaoneshi hali ya kunijali kama mdogo wao. Mimi najitahidi kujisogeza karibu yao afteral mimi kwa mama angu tuko wawili tu, na wao wako wengi, so ninachojaribu kukifanya ni angalau nami niwe najipa amani ya kuwa nina kaka na dada zangu wengi. Kiukweli, sina amani hata kidogo katika maisha kwa sasa pale ninapoona ndugu zangu wa karibu hawaonyeshi kufurahishwa ama kujali juu yangu. Niambieni nifanyeje? Ni hayo tu.......
Share This :

Post a Comment

 

Top