January 29 2013 ndio msajili alithibitisha kwamba mwigizaji Lulu ametimiza masharti yote ya dhamana juu ya kesi inayomkabili ya kuua bila kukusudia na hivyo kumwachia kwa dhamana.....
Lulu na mama yake mzazi wote kwa pamoja waliangua vilio baada ya dhamana yao kukamilika wakati wakiwa nje ya Mahakama kabla ya kuondoka na Lulu kuingia uraiani.
Kabla ya dhamana hiyo kulikwa na tetesi kwamba Lulu angefanyiwa sherehe kubwa ya kupongezwa kuja uraiani.
Kwa mujibu wa ndugu yake wa karibu, Lulu amegoma kufanyiwa sherehe na badala yake jana aliwaomba watanzania wamuombee kwa mungu maana kesi bado inaendelea.....
“Nawashukuru watu wote na nilikua naomba watu waendelee kuniombea sababu hii ni dhamana tu lakini kesi bado ina safari ndefu… nawashukuru wale wote waliokua na mimi kwa hali yeyote ile na zaidi zaidi namshukuru sana Mwenyezi Mungu”....LULU
Post a Comment