Stori: Richard Bukos
VUGUVUGU la kesi ya Kiongozi wa Jumuiya za Kiisalam, Sheikh Ponda Issa Ponda linaendelea kufukuta na watu wengine wametiwa mbaroni kwa kuhusishwa na uvunjifu wa amani.
Tukio hilo limetokea Februari 18, mwaka huu nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam ambapo Sheikh Ponda alifikishwa mahakamani hapo.
Wakati Sheikh Ponda akiingizwa kwenye chumba cha mahakama baadhi ya wafuasi wake walitaka kuingia, wakazuiwa jambo lililowakera na kuanza kufanya vurugu.
Jeshi la Polisi liliwatia mbaroni baadhi yao huku wengine wakiambiwa watawanyike na askari aliyekuwa akitumia kipaza sauti.
“Tunawaomba wote mliofika kwa ajili ya kesi ya Ponda mtawanyike kwa amani, kwani kesi hiyo imeshamalizwa,” alisikika mmoja wa maofisa wa polisi.
Hata hivyo, hakuna uharibifu wowote uliotokea kutoaka na vurugu hizo.
Kesi ya Sheikh Issa Ponda ilitarajiwa kutajwa tena Februari 19, (jana) katika mahakama hiyo.

Post a Comment