Jambo hili linapokuwa linazungumzwa mtaani hasa Jijini Dar utadhani ni masihara lakini lina ukweli ndani yake.
Mwandishi
wetu ambae alikuwa Jijini Arusha hivi karibuni alijionea madai hayo na kupata kisa kizima cha wanamuziki hao
kutotakiwa kukanyaga Jijini Arusha.
Macharii
hao wa Arusha ambao wanasifika kwa ukorofi walimsimulia mwandishi wetu
na kumuorozeshea majina ya wanamuziki ambao wakijaribu kutia pua zao
kwenye ardhi ya Jiji hilo wameisha.
KALAPINA:Kiongozi
wa kundi la Kikosi cha Mizinga chenye maskani yake mitaa ya block 41
Jijini Dar.
Huyu amekuwa kwenye tageti ya masela hao kitambo kufuatia
bifu lake na wanamuziki wa Nako 2 Nako ambapo miaka kadhaa ilioyopita
mmoja wa wanamuziki wa kundi hilo lenye umaarufu mkubwa Arusha alidaiwa
kutekwa na kupigwa hadi kuvunjwa taya na wanamuziki wa Kikosi cha
Mizinga hali iliyoleta uhasama hadi leo licha ya tukio hilo kutokuwa na
ushahidi wa kutosha.
DIAMOND
THE PLATINUM:Macharii hao walisema kuwa licha ya kosa lake sio kubwa
sana lakini wanammaindi kutokana na mwaka jana kushindwa kufika kwenye
onesho la muziki ambalo ilibidi atoe burudani.
Watu wengi walitoa
kiingilio chao tena shilingi elfu kumi kumi matokeo yake hakufika
ukumbini kwa madai ambayo baadae aliyatoa kwenye vyombo vya habari kuwa
ndege ilimuacha.
Waliongeza labda akitaka usalam aende akawaimbie
shoo bure tena uwanjani na kuwaomba radhi watakuwa wameyamaliza.....
BOB
JUNIOR: Utozi ulimponza,Macharii hao walisema kuwa mwaka jana
mwanamuziki huyo alienda kufanya shoo lakini macharii hao
waliamua kumbadilikia kwa kumrushia makopo ya maji stejini pamoja na
mayai hali iliyopelekea kuokolewa na mabaunsa pamoja na
polisi,kisha wakamwambia asirudi tena Jijini humo.......
OMMY
DIMPOZ:Yeye amejipalia mkaa kwenye sakata lake na Lord Eyez la
kumtuhumu kuiba vifaa vya gari ya Ommy hali ililosabasha mwanamuziki
huyo nyota wa kundi la Nako 2 Nako kwenda jela miezi kadhaa.
.
Hali hiyo
ilionekana kuwa kera sana macharii hao na kusema wanamsubiri kwa hamu
kubwa aende A Town wakamletee noma.
Post a Comment