Games

LATEST UPDATES

Monday, July 13, 2015

NILIONGEA NA SHETANI ILI NIWE TAJIRI ... 01

credit: simulizi zangu


 
wazazi waliniita Bella, shuleni nikajiita Bianka. Nilitunukiwa tunu ya urembo, urembo haswa. Hapo mwanzo nilikuwa nikichukia macho ya wavulana waliokuwa wakinitazama kwa uchu. Nilijuwa ulikuwa ni uchu kwa kuwa, sikuwa najitambua wala kupevuka bado. Kioo changu mwenyewe pia sikukiamini kila niipojitazama. Ni wachache walionifuata na kuniambia.
"Bella wewe ni mrembo uliependelewa"
hiyo ndio sababu ya kushinda kwenye kioo na kuutazama huo uzuri. Muda mwingine nilikaa nikijiuliza
"inawezekana wanataka kunichezea? Huo uzuri uko wapi sasa?"
kisha nilikiacha kioo na kukirudia kitabu changu. Ndipo nilisikia sauti ya mama akiniita kutoka nyuma ya mlango.Kumbe mama alikwisha gonga sana mlango mimi sikusikia. Kitabu kilichoitwa KIVULI CHEUSI kiliuteka ufahamu wangu. Aliita mara ya tatu ndipo na mimi nikaupata ulimi wangu.
"bee mama"
nilinyanyuka na kwenda kuufungua mlango. Mama aliniangalia kwa dharau kabla ya kusonya. Sikujali kwa kuwa nilikwishamzoea. Aliingia ndani moja kwa moja na kwenda kukaa kwenye kitan...da changu. Nilipokuwa nafunga mlango nikimfuata alipo, mama aliniambia.
"mwanangu umekuwa"
sikumjibu kitu, nilitabasamu na kumuacha aendele kuzungumza.
"miaka kumi na sita si midogo haswa uzuri ulio nao" nilishituka niliposikia neno hilo kutoka kwa mama, pia sikujibu kitu. Kisha aliendelea
"mwanangu kuna jambo la muhimu nataka kukueleza ili ulifahamu kabla sijafa"
kiukweli mama alinichanganya sana sikujuwa alikuwa ana maana gani. Sikuweza kuongea chochote kwa kuwa sikuwa na lolote la kumwambia au kumuuliza. Nilihisi machozi yakitaka kunitoka. Lakini sikujuwa sababu ya mimi kutaka kulia. Nilimpenda sana mama yangu. Ndiyo, nilikuwa na baba ila mama yangu ndiye alikuwa rafiki yangu wa karibu. Baba hakunijali kama alivyonijali mama. Nilikaa nikimsikiliza kwa makini alichotaka kuniambia.

Mama aliniambia "mwanangu, usikubali hata siku moja kuwa mchawi. Babu yako alinilazimisha kunirithisha mikoba yake nikakataa, amedai kuwa mizimu imekupenda. Yupo katika harakati za kuniua kwa sababu ya kumpinga wewe kuwa mchawi"
niliumizwa sana na taarifa hiyo. Mama alikuwa akiongea machozi yakimtiririka. Nilimbembelea mama huku nikimuhakikishia kuwa siwezi kuwa mchawi. Mama aliniambia
"mwanangu muheshimu sana huyu mzee unayeishi naye"
nikamuuliza "mzee? yupi!"
sikuweza kutambua kama alikuwa akimzungumzia baba.
Ainiambia "mzee Nyegezi, si baba yako Bella, ni mwanaume aliyeyaokoa maisha yangu baada ya mume wangu wa kwanza kutolewa kafara na babu yako" nililia sana nililia kwa uchungu kwa sababu sikujua babu yangu angekuwa na roho ya kinyama kiasi kile. Amuuwe mwanaye kwasababu ya uchawi? Kafara? Kwa faida gani? Unyama ulioje? Nilimchukia babu kwa kuninyima haki ya kumjua baba yangu na mimi kulelewa na baba wa kambo.

Mama aliniambia tena "mwanangu mzee Nyegezi atakulea vyema kama baba yako mzazi. Nina uhakika sina siku zaidi ya saba duniani, lakini nitakapokufa usisahau kusoma kwa bidii na usikubali kuwa mchawi" alinyanyuka na kuondoka. Nilichokuwa nikisoma kikatumbukia nyongo hata wimbo wa Ben po haukuwa mtamu kama nilivyokuwa nikiupenda siku zote. Niliitupa ipod yangu mbali na nilipolala, nikapitiwa na usingizi ulioletwa na kulia sana
.............................
Niliamshwa na upepo mkali uliovuma chumbani kwangu. Upepo niliodhani huenda ungeezua paa la nyumba yetu. Muda mwingine nilihisi kitanda nilichokilalia, kama kilikuwa kinabebwa. lakini hiyo ilitokana na nguvu ya upepo. Nilipotaka kupiga kelele za kuomba msaada, nilijifahamu kuwa napiga kelele kwa sauti ya juu, lakini sauti yangu mwenyewe sikuisikia. Jasho jingi likanitoka. Macho yakatumbuka pima kwa uoga. Ile hali ilipotulia nilitaka kunyanyuka lakini sikuweza kusogeza hata kidole. Nikasikia sauti ya kicheko kikicheka kwa dharau. Nikaangalia mlangoni labda alikuwa ni mama, lakini hakukuwa na mtu. Machozi yalinitoka kwa uoga. Sauti ile ikacheka zaidi na kujirudia rudia kama mwangwi katika chumba changu. Hatimaye nikauona moshi mweusi ukitanda kutoka katika paa na kushuka mpaka usawa wa kitanda. Mbele yangu akasimama mwanaume ambaye sikumfahamu kabisa. Alikuwa amejifunga sanda nyeupe na kuonekana machona pua . Puani aliwekwa pamba mdomo ulikuwa hauonekani. Aliongea na mimi kwa sauti iliyokuwa ikijirudia rudia.
"Bella lazima urithi lazima urithi mikoba"
kisha alisonya, sonyo lililonifanya nipige kelele kwa nguvu mpaka niliamka. Kumbe nilikuwa nimelala. Nilijikuta nikiwa mapajani kwa mama akinifuta jasho lililolowesha gauni yake aliyovaa. Aliniuliza
"babu yako alikuwa anasemaje"
nilishituka, kwa kuwa nilijua fika nilikuwa ndotoni, sasa mama alijuaje? Nilihisi huenda mama alimuona babu. Nikamuuliza mama
"mama umejuaje kama ni babu na mimi nilikuwa naota?"
mama alinicheka kama niliyekuwa nikichekesha. Aliniangalia baada ya kusikitika na kuniambia.
"mwanangu nafahamu yote"
"unafahamu!?" nilishangaa
"ndiyo" akanijibu
"unafahamu nini?"
nilimuuliza huku nikiwa ninakaa kitako kumsikiliza.
Aliniambia kuwa alipokuja kuniamsha ili nikale chakula cha usiku, aliniona nikiweweseka. Akaja na kukipakata kichwa changu huku akiniombea. Ndipo akaisikia sauti ya babu ikiniambia "lazima niirithi mikoba" Aliisikia sauti ya babbu katia ulimwengu wa roho. Nililia sana, huku nikimwambia mama kuwa sitaki kuwa mchawi. Mama alitabasamu na kuniambia
"nakuombea Bella msimamo wako uwe hivyo hivyo"
tulienda sebuleni kupata chakula cha usiku kabla ya kulala tena mpaka kesho siku nyingine mpya. Baada ya kumaliza kula nilimuomba mama aniombee kabla ya kwenda kulala. Tuliomba kwa muda mrefu sana. Mama alivunja nguvu za giza zote na uchawi wa babu yangu. Wakati nikiwa nimefumba macho, nilishituka kuhisi mama amenyamza ghafla na kuanguka chini. Niliogopa. Mama alikuwa anatoa mapovu mdomoni na akigalagala pale chini kama mwenye degedege. Nilimuita baba, mzee Nyegezi. Alikuja na tukasaidiana kumpeleka hospitali. Ulikuwa ni usiku mkubwa hivyo ilikuwa rahisi kwetu kufika mapema na kupewa matibabu haraka. Baada ya daktari kumchukua na kuanza kumshughulikia mama zilipita dakika 30 mpaka alipotoka.
"anaendeleaje!" baba alimuuliza
"nifuateni ofisini"
tulimfuata ofisini huku tukiwa na asilimia chache za mama kuwa mzima. Niliogopa sana.
Tukiwa katika chumba cha daktari. Mimi jasho jingi lilikuwa likinitoka. Kiukweli sikuwa tayari kupokea habari za msiba wa mama. Baada ya daktari kumaliza kuandika vitu fulani katika kadi kadhaa zilizotapakaa katika meza yake, aliinua uso wake baada ya kikohozi kifupi kumpitia.
"poleni sana" alisema
mapigo ya moyo yalienda kasi sana. Yaliende mara tatu zaidi ya kasi ya kawaida. Nilihisi machozi yakianza kustahimili uvumilivu wake na kutaka kuniponyoka. Daktari aliendelea
"ndugu yenu, amepatwa na homa kali sana lakini ni mzima. Tumemuwekea dripu ya dawa hivyo kesho asubuhi muje kumtazama anaendeleaje ila kama mngechelewa? Angekuwa katika hali mbaya zaidi ama mngempoteza kabisa" daktari akaturuhusu kuondoka. Kiukweli niliona kama muujiza mama kupona. Moyo wangu ukiwa na amani sasa na furaha. Tulikuwa njiani tukirudi nyumbani mimi na baba ndipo tulimuona mtu kasimama kando ya barabara. Alitupungia mkono. Baba alisimamisha gari na kumpa lift yule mtu. Baada ya kuingia ndani ya gari, alitusalimu. Baba aliendelea kuendesha gari kwa mwendo wa kawaida tu. Yule mtu tuliyempakia alikuwa mwanaume. Alikuwa muongeaji sana alileta mazungumzo ya hapa na pale
"poleni na mgonjwa" Ghafla alituambia.
Nilishituka sana. Nilishituka kwa kuwa hakuna ambaye alimwambia wapi tumetoka. Mimi sikuzungumza chochote, lakini kwa mshituko mkubwa, baba alisimamisha gari na kumuuliza
"wewe umejuaje?"
yule mtu tuliyempakia alijichekelesha chekelesha pale na kutuambia.
"sikiliza mzee Nyegezi"
moyo ukanilipuka kama ulitaka kunyofoka kifuani. Nilibaki nikimsikiliza. Baba naye alimsikiliza macho yakimtoka pima.
"nafahamu kila kitu kuhusu mama yake Bella" alinyamaza huku akiniangalia mimi "ubishi wake unamponza ubishi utampokonya maisha yake anayoyaringia ubishi unaweza kumletea matatizo makubwa katika kizazi chake na Bella" moyo wangu ulinienda mbio sana mwili ulininyong'onyea nikapoteza nguvu. Nilifiiri sana mtu huyu wa ajabu ajabu alitujua vipi na kufahamu fika siri za familia yetu. Kicheko kilichomlipuka na kurudia rudia kama mwangwi kisha alisonya kabla ya kutoweka na kutuachia moshi mzito mweusi ndani ya gari. SIkujuwa nilifikaje nje ya gari, wala sikukumbuka kilichotokea. Nilijikuta katikati ya barabara nikikimbia kuliko kawaida. Mara chache nilistahimili kujikwaa nilipokuwa nikifanya uzembe wa kutazama nyuma, ndipo nilimuona baba naye akinijia mbio. Aliniita baada ya pumzi kumuishia akiwa amechoka hoi. Nilisimama na kurudi alipo
"baba gari tumeiacha wapi..."
sikujuwa tulikimbia umbali gani hivyo hata gari sikuiona. Baba alikuwa amechoka haswa, ilimbidi akae chini.
"gari.. Gari ipo... Kule" alikuwa amegeuka na kunionyesha tulipokuwa tumetoka ndipo gari ilikuwepo. Baba akanishauri tupumzike kwanza. Baada ya dakika chache tulirudi nyuma lilipo gari. Milango ilikuwa wazi na taa zikimulika huku likiwa limewashwa
"hukuzima?" nilimuuliza
"wewe unajitambua ulitoka vipi"
tulicheka kwa pamoja na kuingia ndani ya gari, tukaondoka kurudi nyumbani. Safari ilikuwa fupi tuliongea mengi ya hapa na pale tukicheka pamoja. Nilipokuwa nikiingia chumbani kwangu, baada ya kufika nyumbani; baba alinishika mkono na kuniambia.
"Hivi bella unafahamu wewe ni binti mrembo sana?"
baba alinishangaza sana. Sawa nilishaambiwa hata na mama, nilianza kuuhisi urembo wangu pale nilipokuwa nikicheka mbele ya kioo na pia rafiki zangu walinihusudu sana na kutamani wangekuwa kama mimi. Iweje baba anishike matiti yangu na kunitomasa kiuno changu? Hapo ndipo nilipoipata ile nguvu ya kuuputa mkono wake na kuutoa kiunoni mwangu.
"baba nakuheshimu kama baba yangu"
neno hilo likaniponyoka. Nilishuhudia mshangao wa kuigiza katika uso wa Mzee Nyegezi. Sikujali niligeuka na kutaka kuingia zangu chumbani. Alinishika tena mkono na kuniambia
"hivi kama mama yako ameshakuambia mimi si baba yako mzazi huoni kama hakuna kinachotuzuia sisi kuwa wapenzi?"
alikuwa akicheka cheka kicheko kilichouudhi. Alinisogelea na kuanza kunitomasa tomasa na mdomo wake kuanza kuunganisha na papi zangu akiwa na nia ya kutaka tubadilishane mate. Nilirudi nyuma baada ya kumzaba kibao na kumuacha akiugulia maumivu na mimi niliingia ndani haraka. Niliufunga mlango kwa ufunguo nikimuacha nje akiropoka ropoka
"mshenzi wewe huna adabu nimekulea mimi siku zote leo unanivunjia adabu mimi? Unanipiga kibao? Nitakuonesha mwanaizaya wewe"
alipotelea chumbani kwake huku akiendelea kubwatuka


+NI HADITHI INAYOTISHA
+HADITHI YENYE UASILIA
+ sijajua itakuwaje kuhusu Bella? atakubali kurithi mikoba?
+hospitali hali itakuwaje alipolazwa mama yake Bela?
+ mzee Nyegezi atamnasa Bella kimapenzi?
Share This :

Post a Comment

 

Top