Games

LATEST UPDATES

Sunday, July 21, 2013

HIVI NDIVYO KALAPNINA ALIVYOONESHA USINITCH BAADA YA KUZUSHA LINAH KABAKWA

Linah Sanga amezikanusha ripoti zilizosambazwa leo kuwa amebakwa na rapper Kimbunga na kudai kuwa ameshangazwa mno na taarifa hizo.

Taarifa hizo zimeanza kusambazwa leo mchana baada ya akaunti ya Facebook inayoonekana kuwa ya rapper Kalapina yenye jina ‘KalApina Kikosi Cha Mizinga’ kuandika:
 
“Mtoto kimbunga amechamba ana leta usela mavi mambo ya kizamani hivi yupo chini ya ulinzi osterbay police kwa kosa la kumbaka msanii lina.”

Baada ya Linah kutafutwa kuhusiana na taarifa hizo akafunguka namna hii
"Kiukweli sijapenda, yaani bora mtu anizushie kitu kingine chochote lakini si suala kama hilo hapo, si suala zuri,” amesema Linah.
 
Amesema jana usiku alitoka na mpenzi wake kwenda kwenye sinema na wakarejea nyumbani salama.


“Sasa sielewi huko kubakwa nimebakwa saa ngapi na nilikuwa na boyfriend wangu labda yeye ndio kanibaka! Maana mtu wanayeniambia amenibaka Kimbunga, huyo Kimbunga hata simjui, namskia tu.
 
Nashindwa kuelewa, kwanini mtu azushe kitu kama hicho yaani ndo nataka kujua source ni nini. Niko fine yaani, kwasababu naelewa ‘it’s not true, lakini nafikiria huyo mtu mpaka kaamua kunifanyia kitu kama hicho, nimemkosea nini au kuna kitu gani, yaani hicho ndio kinaniumiza kichwa.”
 

Share This :

Post a Comment

 

Top