BEAUTIFUL Onyinye, Wema Isaac Sepetu kama kawa ameshuka na mpya ya kumpulizia mbwa wake pafyumu yenye thamani ya dola 120 (zaidi ya shilingi 180,000).
Mkali huyo asiyekaukiwa na matukio Bongo amefunguka kuwa analazimika kumgharamia mbwa huyo pafyumu hiyo kwani ni moja kati ya viumbe ambavyo anavihusudu kupita maelezo.

Kuhusu manunuzi, mkali huyo anayekimbiza kwenye soko la filamu Bongo alisema mara nyingi pafyumu hizo huwa anaagiza kutoka nje au kwa watu wake maalum hapa Bongo ili kuwa na utofauti wa ubora na hadhi yake ya kistaa.
Wema aliendelea kusisitiza kuwa mbwa huyo huwa anampa kampani na wakati mwingine humfurahisha pindi anapokuwa ameboreka au anapokuwa peke yake nyumbani.
“Mara nyingi huwa naagiza kutoka Uarabuni, unajua kule pafyumu zao ni nzuri na ubora wake ni wa hali ya juu,” alisema Wema.
Mkali huyo mara nyingi amekuwa akitumia pafyumu za kuanzia dola 300 (shilingi laki nne na nusu) na kuendelea.

Post a Comment