Games

LATEST UPDATES

Monday, February 11, 2013

VITA YA WAISLAMU NA WAKRISTO YAZUKA TENA HUKO GEITA



Source: Jamii Forums By Ngaliba Dume

Habari zilizopo ni kuwa leo Geita mapigano yametokea kati ya Waislamu na Wakristo (hasa waumini wa AIC).Na hii ni baada ya Wachungaji wa AIC kutenga eneo la Buselesele kwa ajili ya machinjio ya wakristo wao,maeneo ya Katoro na jirani ni vurugu na mtifuano!



Mapambano yanaendelea kwa silaha za jadi, mpaka sasa majeruhi kadhaa wana hali mbaya!


Hali imejitokeza baada ya Wachungaji wa AIC jana kuwatangazia waumini wao kuwa hawawezi kula nyama iliyochinjwa na Waislamu kama sehemu ya ibada,hivyo Wachungaji wakaamua kutenga eneo la Kanisa hapo Buselesele kama machinjio…leo asubuhi wakachinja nyama na kuanza kuwauzia Wakristo, hali hiyo ikawafanya Waislamu kwenda kuvamia eneo hilo lenye “nyama haramu.”


Hali hiyo mpaka sasa imeleta mapigano makali, pikipiki zinachomwa, maduka yanafungwa na shughuli zimesimama.Hali inazidi kuwa mbaya, misikiti inachomwa, mtu mmoja alipotiwa kuuawa mpaka sasa, mchungaji mmoja kala kichapo na pikipiki yake kupigwa kiberiti.


Polisi wa Geita wamezidiwa wanakuja wengine toka Mwanza na Chato! Unaulizwa jina ukitaja la kinyume na waliokukamata unaanza kupewa dose.


Chanzo Kingine: WABHEJASANA

Taarifa za uhakika zilizonifikia kama saa moja hivi iliyopita zinaeleza kwamba mapigano yameibuka na yanaendelea kati ya Wakristo na Waislamu katika mji Mdogo wa Buselesele wilayani Chato Mkoani Geita wakigombania kuchinja.


Ni kwamba jana wakristo walitangaza kwenye mkutano wa hadhara kwamba leo Jumatatu wanaanza kuchinja na kuuza nyama kwenye bucha zao,na wakaitangaza moja ya bucha zilizoko katikati ya soko la Mji wa Katoro kwamba ndilo litakuwa likiuza nyama za wakristo.


Ilipofika asubuhi ya leo majira ya saa 9 waislamu wakapata taarifa kwamba bucha hiyo inauza nyama kwa ajili ya wakristo,huku bucha zao zikionekana kudorora ambapo waliamua kwenda na kuanzisha vurugu kwenye bucha hiyo.


Kwa mujibu wa taarifa hizo tayari zaidi ya watu 10 wamejeruhiwa kwa kukatwa mapanga ambapo mmoja hali yake inaelzwa kuwa mbaya na amekimbizwa ktika hospitali ya wilaya ya geita,tayari polisi wa kikosi maalum cha kutuliza ghasia FFU kikiongozwa na Mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai mkoani Geita wamewasili eneo la tukio.
Share This :

Post a Comment

 

Top