Stori: Mwandishi wetu
BAADA ya kudaiwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Ziwani Kisiwani Pemba, Ahmed Juma Ngwali (pichani) amepora mke wa mtu, mambo mapya yameibuka na ukweli sasa umepatikana.
Risasi
Mchanganyiko limeongea na Mh. Ngwali pamoja na shemeji yake, Mbaruku
Nassoro na kubaini kwamba, Asha Nassoro ni mke halali wa mbunge huyo.
Awali ilidaiwa kuwa Ngwali alimpora mwanamke huyo kutoka kwa mumewe, Khalfan Said Chondoma na kumfanyia mipango ya kwenda Canada.
Pia, ikadaiwa kuwa Ngwali aliwabadilisha ubini watoto wawili wa Khalfan aliozaa na Asha na kuwapa ubini wake.
Akizungumza katikati ya waandishi wetu Bamaga Mwenge jijini Dar hivi Jumamosi iliyopita, Ngwali alionesha hati ya talaka aliyoitoa Khalfan na kumpa Asha mwaka 2010.
Aidha, Mh. Ngwali aliweka wazi kwamba siku zote alikuwa akisema kuwa watoto wa Aisha ni wa Khalfan.
“Mimi nadhani kuna watu wanamtumia huyo jamaa kwa lengo la kisiasa, maana uiislamu unasema mke akipewa talaka moja atakaaa miezi mitatu baada ya hapo anaweza kuolewa na mtu mwingine kama hajarejewa na mumewe wa kwanza, sasa kosa langu nini?” alihoji.
Naye kaka wa Aisha, Mbaruku alisema kuwa Khalfan alimpa dada yake talaka moja, kisha akaoa mke mwingine, mwaka mmoja baadaye ndipo Ngwali alipojitokeza na kumuoa.
“Wazazi wangu wanaijua Dini ya Kiislamu vyema wasingeweza kumuozesha Ngwali kama Aisha angekuwa ni mke halali wa Khalfan,” alisema Mbaruku.
Baada ya kupata maelezo hayo, gazeti hili limeamua kuufunga mjadala huu.

Post a Comment