Pamoja na kuwa na heshima hiyo, Nikki anafahamika kwa jinsi anavyopenda kujihusisha na beef kwa kuwadiss wasanii wenzie ambao wengine hawajahi kumjibu. Rapper huyu wa Kill Your Self amekuwa na uhasama wa muda mrefu na kundi la Weusi ambao amekuwa akiwapiga vijembe mara kwa mara hasa kwa kumlenga zaidi Bonta.
NIKKI MBISHI: WEUSI NI WATU WASIOTAKA ‘CHALLENGE’ KUTOKA KWA WATU WENGINE
Hivi karibuni Nikki Mbishi ameanzisha mfululizo wa diss zinazomwendea Ney wa Mitego na hata kurekodi wimbo maalum wa kumdiss rapper huyo wenye jina lake.
NEY WA MITEGO: ‘SIWEZI KUMJIBU NIKKI MBISHI, NAWEZA NIKAMLEA YEYE NA AKAISHI VIZURI NA KUMKODISHIA SALON YA KUSUKA’
Hata hivyo mashabiki wa Hip Hop wameanza kuonesha wasiwasi na kutopendezwa na muelekeo wa rapper huyu ambapo wengi wanadai anapoteza heshima yake.
Wiki hii kupitia ukurasa wa Facebook Nikki aliandika kile alichosema ni mashairi kwenye wimbo wa Ludacris yasemayo: Lord Forgive me for HIP HOP BEEF and forgive me for my DRAMA.
Kufuatia post hiyo, Uisso Ze HardShzee ambaye ni mmoja wa marafiki wa Nikki kwenye mtandao wa Facebook alimwambia: sure bro una drama sana,kuwa makini sio ishu ya kuendekeza hizo coz ni 2 sided. You better focus on music 4 real mbona unaweza tena sana tu.Mtazame Moko,Nash,Mansulii,Stereo the only thing they know is kusaka chamb n doing gud music for their fans, huwackii
wakimzungumzia mtu kizembezembe tht’s why heshima kutoka kwa fans inaonekana, But if daily you think of what new drama to impress fans n pay their attention,maan one day it will cost u directly or indirectly. Do music Mbishi mbona unaweza sana.”
“We Nick hata sijui niaje,” aliandika mwingine aitwaye Nicko Chacha. “Hivi mkishindaga na mtu kama Fid huwa mnajifunza nini?au mnajifunzaga kuandka mashairi tu, acha izo! We una ishu za ajabu sana watu unaofanya nao beef hawakufikii hata kidogo ila uropokaji wako hadi watu wanakuchukulia poa sana. Ungekua tofauti usingekua hapo ulipo, wenzako mn wabovu ila hawakurupuki kama wewe na wanajichukulia max, acha ishu za ajabu wewe. Hivi hata wana wa karibu ndo wanavokushauligi? Hebu fuata misingi ya Ngosha wewe. Ngosha si mropokaji, ishu nyingine zinakua nyuma ya pazia tu sisi tunaofuatilia muziki tutajua, we unazianika hadi sio ishu tena.”
Naye Geofrey Deaver Bulenga aliandika, “oya mwambieni ukweli nikki uwezo anao ila aachane na beef utauza halafu mwisho watu watakuona bwege. Kuwa star sa hizi haimanishi huwezi kuchuja, sasa ukichuja utaacha nini kwa mashabiki, mipasho au nini? Tabia ya kiume unamwambia ukweli mtu akimaind kivyake lakini anaboa kila time Nikki mbona Zillah, Ngwea, Stamina wanauza na sio kwa beef kama wewe we ndio unajua sana ehh.”
Leo kupitia Facebook rapper na aliyewahi kuwa mtangazaji wa Clouds FM, Rueben Ndege aka Nchakalih ameandika kitu ambacho kwa haraka haraka alikuwa amemlenga Nikki Mbishi ama rappers wengine wanaoependa kuropoka.
“EMCEE MWENYE SKILLZ NA MWENYE IQ ANAJUA KUCHAGUA NI KIPI CHA KUSEMA NA NI WAPI PA KUKISEMA KITU HICHO….hakuna kitu kinauma kama kumuona emcee ambae unamuheshimu sana uwezo wake…akiendelea kufanya watu waache kuzungumzia uwezo wake na kazi zake…na wabaki wanajadili HULKA AU TABIA.”
imeandikwa na Abubakar Kisukari
Post a Comment