Games

LATEST UPDATES

Thursday, February 7, 2013

Dalili kumi za kukuonyesha kuwa mwenzi wako ana-cheat...

Je utagunduaje kuwa Mwenzi wako ana Cheat na mtu mwingine?

Uzoefu wa wengi waliopitia katika sekeseke hili unaonyesha kuwa kuna dalili kama 10 ambazo zitajionyesha na kukufanya uwe na hisia kuwa unaibiwa:

1. Mwenzi wako anakuwa more critical au na ubishani usio hata na tija katika mambo madogo nay a kawaida. Sababu ni kuwa kuna mpenzi mpya ambaye ana share naye hisia zake za kimapenzi na matokeo yake ni kuwa umuhimu wako kwake unapungua na hivyo hajali chochote anachokuambia wala hayuko sensitive na feelings zako.

2. Unapowauliza juu ya habari zao mfano “Ulikuwa wapi?” au mambo ya kimsingi wanakuwa hawaeleweki, au wanajifanya kukasirishwa au kuleta arguments zisizo na tija.. 

3. Ukiona mwenzi wako anakimbilia bafuni kuoga mara tu akiingia nyumbani hiyo pia si dalili njema. Madhumuni yake huwa inakuwa ni kuondoa harufu ya mtu mwingine, au marashi ya mtu mwingine au hata harufu iliyobaki wakati wa majambozi.

4. Kama mwenzi wako anatumia Computer na wewe unaingia anaamua ama kuhama nayo au kuifunga au kufunga windows haraka na kasha anaonekana a bit nervous na kudivert mazungumzo mara aulizwapo mbona unahama au unafunga computer?

5. Mwenzi wako anajiweka pembeni anapopokea simu Fulani Fulani au anapotuma au kupokea SMS Fulani. Anakuwa hachezi mbali na simu yake. Wakati mwingine analala nayo, kwenda nayo washroom, kuilock bila ulazima au unapoomba utumie simu yake kwa sababu muhimu kukataliwa bila sababu za msingi

6. Mambo ya kujiweka soap soap au kujirembesha yanabadilika, hasa katika Nyanja za perfume perfume; hairstlyles, smartness, nk.

7. Grooming habits pia inabadilika tofauti na ile iliyozoeleka ambayo labda ulikuwa unaifurahia. Hasa mavazi, na kujirembesha. Mwonekano wake anapenda ubadilike ili avutie zaidi, mara nguo nguo mpya, viatu nk nk. 

8. Hobbies, interests na mipangilio ya maisha inabadilika na inakuwa tofauti na ulivyozoea. Hiyo inamfanya aendane na mpenzi wake mpya.

9.Ghafla mwenzi wako anakuwa busy au na ratiba zisizoeleweka tofauti na mazoea ili mradi ratiba hiyo isimweke karibu na wewe au na nyumbani. Bila ya shaka hii ni kumpa wasaa wa kuwa na mpenzi wake mpya. 

10.Kihisia na kimapenzi anakuwa mbali na wewe na interest inapungua kabisa kama siyo kufa. Hii ni a very strong sign hasa pale hata maongezi yanapungu na hakuna hata mambo ya kushare pamoja tu ila yale ya msingi, less affection, less cuddling, less sex and less emotional attachments

Kama mwenzi wako anazo baadhi ya dalili zilizotajwa bila ya shaka suspicion zako zinaweza kuwa za kweli na inabidi uzifanyie kazi za “Ki-Intelligensia” ili kupata uhakika au ushahidi.

Maswwali la kimsingi ni: 

1. Je utapataje ushahidi wa uhakika katika mambo yaliyotajwa?

2. Je, kuna dalili zozote za ziada zaidi ya zililzotajwa ambazo zinaweza kuwa ni kiashirio kuwa unaibiwa?
Share This :

Post a Comment

 

Top