Games

LATEST UPDATES

Monday, January 28, 2013

Dua La Afrika Mashariki yasalia mikononi mwa DRC

Timun ya Taifa ya Soka na DRC
Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo leo inajianda kwa mechi yao ya makundi ya michuaano ya kuwania kombe la mataia ya Afrika, dhidi ya Mali.
Timu hizo mbili ni sharti ishined mechi hiyo ya Kundi B, ili ifuzu kwa robo fainali ya mashindano hayo.
Endapo timu hizo mbili zitashona nguvu, Mali, huenda ikafuzu kwa robo fainali, ikiwa mechi nyingine ya Kundi hilo kati ya Niger, itamalizika huku timu hizo zikitoshana nguvu au Ghana ikiibuka na ushindi.
DRC, inashikilia nafasi ya tatu katika kundi hilo baada ya kutoka sare mechi zao mbili za kwanza.
Timu ya taifa ya Mali
Kocha wa Congo, Claude LeRoy, anasema kikosi chake kinakabiliwa na kibarua kigumu kuipiku Mali.
‘‘Ushindi pekee ndio utakaotuwezesha kufuzu kwa robo fainali’’ alisema LeRoy.
Ni timu hiyo ya Congo, pekee ndiyo iliyofuzu kwa fainali hizo mwaka huu, kutoka kanda ya Afrika Mashariki na Kati.
Hata hivyo makocha wa timu hizo mbili watakuwa na wachezaji wao wote katika mechi hiyo.
Kocha huyo wa Congo amesema amewahimiza wachezaji wake kucheza mchezo wa kushambuliaili kuimarisha nafasi yao.
Naye kocha wa Patrice Carteron, amesema nia yao kuu ni kutoka sare, ili kujihakikishia nafasi katka raundi ijayo na ni lazima tusahau, kipigo tulichopata dhidi ya Ghana na kuangazia mechi dhidi ya Congo.
Share This :

Post a Comment

 

Top