Games

LATEST UPDATES

Sunday, December 23, 2012

POH MONTANA - ON TOP_(Prod_by _OMMYRUNNER_sOUNd kALi_mUSic-)

Poh Montana ni mwanamuziki kutoka mkoa wa Mara manispaa ya Musoma kata ya kitaji. Alianza harakati za muziki mwaka 2002 alipohitimu shule ya msingi Mwembeni iliyopo huko Musoma na kuhamia jijini Dar es Salaam ambako alikamilisha elimu yake ya sekondari.
      Mnamo mwaka 2010 akiwa katika chuo kiuu kishiriki cha Tumaini jijini Dar es Salaam ndipo alikutana na watu kama Mtani ambaye ni producer na kiongozi wa kundi la Stunt Hits, Yommy Raw na Blessing Sophie Malet a.k.a Brick Lewinsky na kuunda kuunda kundi la NOTED. Lakini kama ilivyo ada katika makundi mbalimbali huwa kila mmoja hufanya kazi peke yake(solo artist).
      Mnamo December 2012 Poh Montana alikutana na producer Ommyrunner katika studio za Kali Music zilizopo Mbezi beach jijini Dar es Salaam na kurekodi track yake ya kwanza iliyo kwanda kwa jina la On Top ambayo ni track iliyomtambulisha vizuri kwenye tasnia hii ya muziki wa kizazi kipya.
      Vile vile Poh Montana ni mwanamuziki mwenye uwezo wa kupita style ya (Modern Hiphop) kama aliyoifanya kwenye track hii yaani anaimba na kuflow. Kwa mawasiliano zaidi tembelea ukurasa wake wa Facebook; Prominent Paul au fan page yake ya Poh Montana na kupitia twitter; @Paul thrills
Share This :

1 comment :

 

Top