Games

LATEST UPDATES

Wednesday, January 23, 2013

NILIONGEA NA SHETANI ILI NIWE TAJIRI .. 6


MUANDISHI STALLONE JOYFULLY
MAWASILIAO +255 654 846 084

ILIPOISHIA....

Babu akaniuliza Swali
“je upo tayari kuurithi ufalme wangu mara nitakapokufa?”
aliniambia huku akiwa na anatokwa na machozi ya damu. Sikuelewa hali hiyo ilimaanisha nini ila nilishindwa kukubali haraka haraka. Lakini pia sikupenda kufa mapema kama alivyokufa mama. Nilitambua fika ule ndio ulikuwa mwisho wa kuonana na mama yangu. Mama aliondoka katikati yetu na kuvalishwa kaniki nyeusi kama walizovaa wengine wengi katika kjiji hicho. Baada ya kutafakari sana kwa dakika chache baadaye nilimjibu babu.

HAYA ENDELEA SASA...

“babu naogopa kuwa mchawi”
Nilijibu kiuwoga. Nilijibu nikiwa namaanisha kweli ninaogopa kuwa mchawi. Tuliendelea kutembea katika mitaa mbalimbali ya kijiji hiko cha wachawi.
Babu alitabasamu na kunigeukia
“mjukuu wangu uchawi hauna madhara yoyote”
“babu hauna madhara?”
Niliuliza kwa mshituko. Babu alicheka na kunijibu kifupi
“ndiyo, hauna madhara yoyote”
“babu mimi siwezi kula nyama ya mtu, kunywa damu ya binadamu wala mnyama, siwezi kuua. Babu sitaki kuwa mchawi”
babu alizungumza na mimi kwa upendo hata nikajisiia faraja
“mjukuu wangu, nafasi niliyo nayo ni kuwaadhibu wale wanaokiuka masharti ya mkuu wa ulimwengu huu hivyo wewe nawe utakuwa vivyo hivyo kama utakubali kurithi nafasi yangu”
nilimuomba babu anipe muda nitafakari jambo hilo kwa muda. Babu alinipa masaa machache hivyo alidai kuwa angelifuata jibu lake usiku.
Tulipokuwa tukiendelea kutembea tembea, nilishituka kumuona mtu ninayemfahamu kabisa. Alikuwa ni mtu mmoja maarufu huko duniani. Alikuwa ni mwanasiasa aliyeogopwa sana na vyama pinzani, pamoja na chama chake. Nilisikitika kumuona akiwa pale. Amechoka, amekuwa mweusi tofauti na alivyokuwa kule duniani. Nilipotaka kuzungumza naye, babu alinizuia.
“hapana Bella, wewe bado hujawa na nguvu za kuweza kuzungumza na misukule”
nikamuuliza babu
“kwani huyu amefanya nini mpaka yupo mahali hapa?”
“yeye alitolewa kafara na mume wake, mume wake ni mfanyabiashara maarufu lakini yupo katika chama kimoja maarufu kinachotoa kafara na kumwaga damu kwa sababu ya utajiri”
nilitetemeka sana niliposikia hivyo. Baada ya muda, nikatamani kuzunguka zunguka tu mule katika kile kjiji cha Gamboshi ili niweze kuwaona watu mbalimbali ambao ninawafahamu.
Tulipita katika kijiji duni ambacho niliwaacha wale misukule sasa tukaingia katika sehemu yenye uafadhali wa maisha katika shemu hiyo ya Gamboshi.
Babu alinieleza
“kule tulipopita mwanzo, ndipo wanapoishi misukule. Lakini huku ndipo ilipo ngome yangu na wachawi wengine wakubwa huko duniani.”
mbele ya majumba mbalimbali ya kifahari. Yaliyojengwa kiufahari. Niliuona mji Fulani ulikuwa uking’aa sana. Ulikuwa ni mji uliokuwa ukiwaka taa zilizotowa mwanga mkali hata kufanya niuone mji ule ukipendeza sana.
Nikamuuliza babu
“kule ni wapi na kuna nini?”
Babu hakunijibu kitu na kunieleza ile si sehemu nzuri kuifikiria wala kutamani kwenda. Alinieleza, miaka mingi sana iliyopita ufalme wa falme ile ilijaribu kutaka kupindua tawala ya mkuu wao na kushindwa. hivyo ilijitenga nao na kuwa maadui wakubwa baada ya urafiki uliokithiri na kujikita katika ndani ya mishipa yao ya damu kabisa, kupoteza mvuto. Sikutaka kuendelea kuuliza zaidi lakini nilihisi jambo kuhusu mji ule niliouona. Mji ule na hapa Gamboshi tulipo, kuliteganishwa na shimo moja refu liliokuwa likitokota uji mzito wa moto. Tofauti ya mji ule na huu wa ngome ya babu ilipo, ilikuwa ule ulipendeza na uling’aa sana lakini huu wa babu ulififia na kuwa kama wenye giza Fulani lisiloeleweka. Babu alinitoa hapo na kunionesha sehemu ambayo mkuu wao alikuwa akiishi.
Alinieleza
“mjukuu wangu, sehemu hii ni takatifu sana. Watu wote maarufu uwajuao huko duniani, huja mahali hapa kumuomba mkuu wetu utajiri na kusafisha nyota zao ili waweze kukubalika zaidi na zaidi.”
“ninaweza kumuona?”
niliuliza
“hapana, bado hujafikia viwango vya kukanyaga sehemu ile”
tuliondoka mahali hiyo na kurudi kule kwa awali. Kule kulipochosha. Kule niliposhuhudia misukule ikifanya kazi kwa bidii. Kule ambapo naamini ningemona tena mama na nimuage kuwa ipo siku nitarudi kua kumtoa.
Nilimuuliza babu
“hivi hawa hufanya kazi kwa muda gani”
babu alicheka sana na kunieleza kuwa
“hawana mapumziko, hufanya kazi usiku na mchana na hupumzika mara moja tu kwa siku” alinyamaza baada ya kumeza mate kasha aliendelea kunieleza “wakati ambao umepangwa wa wao kula tu”
“na huwa wanakula nini?”
“unga na funza, ndio chakula chao kikuu”
nilishangaa sana, ghafla machozi yalinitoka. Nilihuzunika kwa kuwa nilifahamu mama yangu naye alikwisha kuwa msukule. Hivyo chakula chake nacho kingekuwa ni hicho hicho. Nilimlaumu babu kwanini alimuuwa mama yangu. Nililia kwa uchungu huku nikikimbia kusikojulikana. Nilikuwa sijuhi wapi naenda ila nilipishana na misukule na vile viumbe vilivyopaa kama ndege lakini wakiwa na maumbo ya binadamu. GhaflaMbele yangu nilikutana babu akinicheka kwa sauti ya juu sana.
Aliniambia
“Bella huku huna pa kunikimbia”
“babu nakuchukia, nakuchukia kuliko navyomchukia shetani”
ghafla babu alinipiga kibao kilichonifanya nipoteze fahamu. Fahamu iliyonitoa katika ulimwengu wa Gamboshi na kunirudisha duniani. Nilijikuta nikiwa katikati ya watu wengi. Watu waliokuwa wakilia wakinamama wamejifunga kanga zao. Wengine wakinipepea huku wakilia kwa uchungu wakiliita jina la mama yangu.
niliposhituka nilipiga chafya mara tatu mfululizo. Watu walijawa na mshituko. Niliwaona wengi wakiwa na maswali mengi sana juu ya kifo cha mama. Mimi pia nilianza kulia kwa uchungu. Nilifahamu fika sitoweza kumuona tena mama yangu katika ulimwengu huu wa kawaida. Watu walinibembeleza lakini niliona kama walikuwa wakiniongezea uchungu zaidi. Walimuita Mzee Nyegezi.
Mzee Nyegezi alikuwa akizungumza na askari polisi waliofika eneo la nyumbani kwetu. Watu walikuwa wamejaa sana.
Hakika kifo cha mama kilishitua wengi.
Mzee Nyegezi na wale askari, walisubiri ninyamaze kulia kisha waniulize maswali kadhaa.
“pole sana binti”
alizungumza askari mmoja aliyevalia sare zake.
“salama”
kwikwi ilinibana, lakini nilijibu hivyo hivyo. Wakati huo huo ambao askari wakiendelea kuzungumza, ghafla niliisikia sauti ya babu yangu ikizungumza na nafsi yangu
“usiwaeleze chochote askari kuhusu kifo cha mama yako, wajibu hufahamu kitu”
nilipopata kigugumizi cha kujibu kutokana na sauti niliyoisikia, macho yangu yakapata mshangao zaidi nilipomuona babu mbele yangu. Alikuwa kwenye msiba huo kama waombolezaji wengine wa kawaida.
“unaweza kutueleza chochote ulichokiona?”
askari mmoja akalirudia Swali aliloliuliza zaidi ya mara tatu. Sikulisikia kutokana na uwoga na nilijifanya sikuliskia kwa kuwa jibu walilotaka sikuwa tayari kuwajibu.
walinipa muda wa kupumzika zaidi. Huku nikisikia kuwa, mwili wa mama upo hospitali kwa ajili ya uchunguzi.
bado nilikuwa katika woga zaidi. Watu mbalimbali waliingia katika chumba nilichomo kunipa pole. Nilimuona Jordan mpenzi wangu. Nilimuona Bertha rafiki yangu na wanafunzi wenzangu wa shuleni. Dakika chache baadae aliingia mwanamke fulani mwenye mwili mpana na uso wa mviringo. Uwazi Fulani katikati ya meno yake ukamfanya awe na mwanya hata akapendezesha kwa jino la dhahabu. Alijitanda kanga juu, chini akakivaa kitenge kutoka kongo.
sikuwahi kumuona hata siku moja.
Aliniambia
“pole sana Bella”
nilikuwa niimtazama kwa makini bila kukumbuka ni wapi niliwahi kumuona.
Nilimjibu
“asante, sijuhi niliwahi kukuona wapi?”
“Gamboshi,”
hapo hapo nilipoteza fahamu na kuisalimia sakafu kwa kuibusu.

-HAYA SASA WATU WA GAMBOSHI WAMEANZA KUMSUMBUA BELLA
-NINI KITATOKEA KATIKA CHUMBA ALICHOMO BELLA NA HUYO MAMA KUTOKA GAMBOSHI?
LIKE NYINGI, KOMENTI UKITOA MAONI YAKO, SHARE KWA WINGI IKIWA WEWE NI SHABIKI NAMBA MOJA WA HADITHI HII
Share This :

2 comments :

 

Top